Sunday, 31 August 2014

MAMA SALMA AWAFUNDA WALIMU

Mama Salma awafunda walimu
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Salma Kikwete, amewataka wadau wa maendeleo kuzisaidia shule za sekondari za Wama na Kayama zilizoanzishwa na taasisi hiyo ili kuwezesha watoto kuondokana na umaskini.

Mama Salma alitoa wito huo jana wakati hafla ya kuwapongeza walimu ambao wanafunzi wao waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana na hivyo kuwataka waongeze juhudi katika mafunzo ili kufikia nafasi ya tano kitaifa.
“Hongereni sana kwani mmefanya kazi nzuri , tunatambua kazi ya ualimu ni wito kwa kumbalidisha mtu kutoka kutokujua hadi kujua kitu fulani, tufanye kazi katika miito ya ualimu na kuzidi kuzifanya Wama na Kayama kuwa shule bora katika Tanzania hii,”alisema.
Alisema anayo furaha kwa matokeo mazuri kwani hakuna daraja la sifuri na kwamba kati ya wanafunzi 68 waliomaliza, 48 wamefanikiwa kujiunga na kidato cha tano na baadhi yao wameendelea katika shule yao kwa michepuo ya CBE na ECA.
Kwa mujibu wa Mama Salma, wanafunzi 19 walipata daraja la nne, 19 la tatu, 20 la pili 20 na 10 daraja la kwanza 10, hivyo kushika nafasi ya 109 kitaifa na nafasi ya 14 kimkoa.
Aliongezea kuwa, WAMA imefanikiwa kutoa huduma kwa watoto yatima zaidi ya 1,000 kwa shule za sekondari na 14 wa Chuo mpaka sasa.
Mama Salam alizipongeza pia baadhi ya taasisi kwa kuwachangia wakapata mabweni, maabara na madarasa, akisema imewawezesha kuwa karibu na wanafunzi na kuepusha vishawishi kwa watoto wa kike

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!