Saturday, 30 August 2014

Jeshi la Lesotho asubuhi ya leo linadaiwa kufanya uasi ambao huenda ukadondosha utawala uliopo madarakani - Wamezingira Ikulu, Wameyateka Makao Makuu ya Polisi na kukata mawasiliano ya Redio na Simu nchini humo


Jeshi la Lesotho


Ripoti kutoka Taifa la kusini mwa Afrika Lesotho zinasema kuwa jeshi limezingira makao makuu ya polisi na kuzuia matangazo ya radio pamoja na mtandao wa simu katika mji mkuu wa Maseru.

Shirika la habari la AFP limemnukuu waziri wa habari Thesele Maseribane akisema kuwa milio ya risasi ilisikika na kukilinganisha kisa hicho na jaribio la mapinduzi .
Uchaguzi ambao haukukamilika nchini humo miaka miwili iliopita ulisababisha kuundwa kwa serikali ya muungano isio dhabiti.
Licha ya mazungumzo ya kuleta amani mnamo mwezi Juni ,hali ya wasiwasi ilitanda huku majirani wa taifa hiilo wakionya dhidi ya mbinu yoyote isio ya kikatiba.

Taifa hilo limezungukwa na Afrika kusini na hutegemea sana jirani yake kwa mali asli pamoja na ajira.
CHANZO: BBC

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!