Friday 1 August 2014

ISRAEL: HATUTATOKA GAZA HADI NJIA ZA CHINI KWA CHINI ZIHARIBIWE KABISA!

Israel inasema kuwa haitaondoka Gaza hadi iharibu njia za chini kwa chini
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa Israel imeamua kuyaharibu kabisa mahandaki na njia za chini ya ardhi zilizojengwa na wapiganaji wa Palestina-Hamas, katika mipaka yake huko Gaza.


Amesema uharibifu huo utatekelezwa na majeshi ya Israeli kukiwa au kutokuwa na muafaka wa kusitisha mapigano.

Netanyahu amesema hayo huku Serikali ya Israel ikishikia kani kuwa kuwa itaendeleza mashambulizi katika eneo la Gaza licha ya shutma za kimataifa kufuatia shambulizi la shule moja ya umoja wa mataifa ambapo takriban watu 15 walipoteza maisha yao.
Mwanamke akiomboleza Gaza
Msemaji wa serikali ya Israel amesema kuwa wataomba msamaha iwapo watabaini kwamba shambulizi hilo, lilitekelezwa kimakosa na wanajeshi wa Israel.
Umoja wa mataifa umesema kuwa ni wazi kwamba ni jeshi la israel ndilo lililorusha kombora hilo katika shule hiyo ambapo zaidi ya raia elfu tatu wa Palestina walikuwa wameomba hifadhi.
Licha ya malalamiko kutoka kote duniani kuhusiana na idadi kubwa ya vifo vya
Njia za chini kwa chini za Hamas ambazo Israeli inalenga kuharibu
Mashambulizi ya Israel kutoka angani na nchi kavu yamerindima kwa milipuko ya mizinga na ndege za kivita.

Na sasa Israel inajiandaa kwa vita zaidi baada ya kuwaamuru wanajeshi wa akiba kujiunga na jeshi la taifa. Katika ukanda wa ngaza ni kilio na majonzi makubwa..
BBC.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!