Wednesday, 27 August 2014

BAMIA HUSAIDIA WENYE VIDONDA VYA TUMBO

Unafahamu kuwa kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali?
Mtandao wa healthandcure.com unawanukuu wataalamu wa afya wakieleza kuwa watu wanaosumbuliwa na maradhi kadha wa kadha ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.

Wataalamu hao wanaendelea kuzitaja faida nyingine zinazotokana na ulaji wa bamia ni pamoja na kuboresha uwezo wa macho kuona.
Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na beta carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona.
Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini.
Pia hudhibiti pia kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta.
Husaidia pia kulainisha choo. Vilevile ni mboga ambayo kwa Waafrika huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza.
Wataalamu wanaeleza kuwa ina virutubisho vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo.
Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!