Monday, 14 July 2014

WENYE HASIRA WAMEDEKEZWA WATAUA HATA "MALAIKA"

Photo: Habr ndg huyu ndye mwizi wa bodaboda raia walivyo fanya kaz yao bada ya kukamata
KATI ya taarifa nilizosoma wiki hii zikanisikitisha, mojawapo ni iliyohusu mwanafunzi wa mwaka wa nne wa Chuo Kikuu cha Ruaha , mkoani Iringa, Daniel Lema; Aliyeuawa kwa kuchomwa moto.
Masikini, alijikuta akihukumiwa isivyo haki na watu wanaojibambika jina la ‘wenye hasira kali’. Eti walidhani ni mwizi. Polisi imethibitisha hakuwa mwizi. Hakupewa nafasi kujieleza. Hawakujali kwamba hakuwa na silaha yoyote.



Badala yake, walimwadhibu kwa kumchoma moto mwili wake. Mauti yalimkuta hospitalini. Mungu amweke mahali pema peponi. Si tu Daniel ambaye tuhuma zimesababisha apoteze maisha.
Wapo watu wengi wanaathirika na mtindo huu ulioibukia wa watu kuadhibu wenzao kwa kofia ya ‘ wenye hasira kali.’ Siku hizi, ukishaitiwa ‘mwizi’, ujue hiyo ndiyo tiketi yako ya kuaga dunia. Ukibahatika, basi utaachwa na ulemavu wa kudumu.
Nimewahi kusimuliwa, msichana aliyekosana na mpenzi wake. Alipiga kelele za mwizi. Haikuchukua muda, kijana wa watu akashambuliwa na kuuawa na ‘wenye hasira kali’. Siku hizi hata dereva akishagonga mtu barabarani, hapaswi kusimama eneo la tukio.
Vinginevyo, anaweza kuuawa na hao wanaochukua sheria mkononi. Kali zaidi, waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda nao wameamua kujiundia ‘dola’. Hutoa hukumu papo kwa hapo pale mwenzao anapokutwa na masahibu hususani kugongwa.
Bila kujali kwamba wao pia ni wasababishi wakubwa wa ajali, ikitokea mmoja wao akagongwa na gari, humvamia dereva husika. Nimewahi kushuhudia dereva aliyepewa kipigo mithili ya kibaka baada ya kumgonga bodaboda ambaye hata hivyo kosa lilikuwa ni la mwendesha pikipiki.
Bodaboda walitumia matofali, mawe na miti kumponda dereva huyo wa gari dogo wakati watu wakishuhudia. Hakuna aliyethubutu kuingilia kati.
Sina hakika kama alipona. Haya ni mambo yanayohitaji kukemewa kwa nguvu zote. Hata hivyo, nieleweke wazi, sitetei uhalifu hata kidogo.
Nafahamu wazi mtu yeyote aliyewahi kuibiwa, kuvamiwa au kufanyiwa unyama wa aina yoyote, hutamani waliomfanyia jambo hilo, wapate adhabu kubwa duniani ikiwemo hata kuuawa.
Hata wale wanaoamini katika msamaha, si jambo rahisi kwake kusamehe kibaka, jambazi, mwizi au mbakaji aliyekudhuru au kumdhuru ndugu, jamaa na rafiki.
Hushangilia akisikia kibaka, jambazi au mbakaji kapigwa au kuchomwa moto na watu wenye hasira kali. Hapo mafundisho ya samehe ‘Saba mara Sabini’, wengi kidogo huyakinga kisogo.
Lakini sasa inapokuja kwamba, wapo baadhi ya watu wasio na hatia wanaohukumiwa kama ilivyotokea kwa Daniel, ndipo inakuja haja ya kukemea vitendo hivi vya kuchukua sheria mkononi.
Yamkini, zipo hoja ambazo zimekuwa zikijengwa na wanajamii kuhalalisha mauaji kwa watuhumiwa wa uhalifu. Miongoni mwake ni kwamba, baadhi wakikamatwa na vyombo vya dola, huachiwa hata bila kufikishwa mahakamani na kuendelea kutamba mitaani.
Inadaiwa wengine hata baada ya kupelekwa mahakamani, ama kesi huchukua muda mrefu bila hukumu kutolewa au huachiwa huru. Pamoja na kwamba hoja hizo zinaweza kuwa na mashiko, haiondoi ukweli kwamba baadhi ya watu huuawa kutokana na visa, uadui binafsi, kukurupuka na ukatili kwa mwavuli wa hasira kali. Ikumbukwe leo wewe ni msafi mithili ya malaika.
Unachukia uhalifu kama ninavyouchukia. Unaunga mkono wezi, vibaka, majambazi, wabakaji wauawe kabla ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ukiamini watakoma kufanya vitendo hivyo. Lakini kumbuka iko siku, wewe pia yanaweza kukuta ya kijana Daniel.
Inawezekana ukakorofishana na ndugu, jamaa na hata rafiki, akakuitia mwizi. Pia inawezekana uko mtaani mtu akaporwa, ukafananishwa na kibaka .
Siyo tu hivyo, unaweza ukawa dereva na umezingatia sheria za barabarani, lakini ukasababishiwa ajali ukagonga mtu na hatimaye kushambuliwa na wenye hasira kali.
Sikatai kwamba hasira na chuki kwa wahalifu, ndivyo huchochea watu kuamua kufanya hivyo. Lakini suala hili liangaliwe kwa mapana bila jazba na ushabiki. Ifahamike, Mahakama pekee ndiyo yenye uwezo kubaini mhalifu.
Kama polisi na mahakimu, baadhi yao hukiuka maadili kwa kulinda wahalifu, ni vyema utafutwe mwarobaini wa tatizo hilo ikiwemo kuwaadhibu lakini bila kuhalalisha au kubariki jamii kuchukua sheria mkonon

1 comment:

Anonymous said...


aziz bilal03:24


1
Reply

Maskini huyo kijana kadhulumiwa haki yake ya kuishi duniani wahusika wote lazima wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria na kujibu mashtaka ya mauaji kwa kukusudia,ka huyo marehemu angelikuwa ni mtu toka family yangu yaani ndugu yangu,yaani hivi sasa tayari ningelikuwa nimekuwa mwehu na mimi ningelifuatilia na kuchukuwa sheria mikononi mwangu ka walivyomfanyia ndugu yangu.Huu udhalimu serikali lazima iingilie kati.criminals wanamuuwa ambaye labda angelikuwa lawyer mkubwa sana na labda angeliweza saidia wengi.Inasikitisha na kuuma sana.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!