Wednesday, 23 July 2014

WANAFUNZI WANUSURIKA KUFA BAADA YA MABWENI KUTEKETEA KWA MOTO!


Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo(Jumatano) asubuhi.


Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kulifikisha wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ametembelea shule hiyo na kiahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.Gharama za kuwasafirisha ni shilingi laki Saba.
Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kwa habari za Jimbo la Monduli tembelea

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!