Tuesday, 15 July 2014

MTOTO ATUMBUKIA KISIMANI AFARIKI

MTOTO Omari Hamduni (3) mkazi wa Keko Magurumbasi jijini Dar es Salaam, amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo alisema kifo hicho kilitokea jana saa 5 asubuhi jirani na eneo alilokuwa akicheza mtoto huyo.
Alisema mama wa mtoto huyo alikuwa akifanya shughuli nyingine za nyumbani ndipo ghafla aliposikia kelele za watu waliomuona Omari akitumbukia kisimani.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, mtoto huyo aliokolewa, lakini alifia njiani akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke.

TZ-DAIMA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!