Monday, 14 July 2014

MTOTO ALIYEKUFA "AFUFUKA" KWENYE MSIBA WAKE


Waombolezaji nchini Ufilipino walipatwa na mshituko, pale mtoto wa miaka mitatu aliyekuwa "amekufa" kuzinduka wakati wanampeleka mazikoni.
Kwa mujibu wa gazeti la Metro -mtoto huyo kutoka Aurora, Zamboanga del Sur, alitangazwa kufa siku ya Ijumaa, na maziko kupangwa Jumamosi mchana.
Lakini wakati wa shughuli ya msiba, ndugu na marafiki walishtushwa wakati mtoto huyo "alipofufuka".
Watu walianza kurekodi tukio hilo baada ya padre aliyekuwa akifanya misa kugundua kuwa mtoto huyo amejisogeza, kabla ya kufungua macho.
Video ya tukio hilo imewekwa kwenye YouTube.


1 comment:

Anonymous said...



aziz bilal03:15


1
Reply

Hakuna cha ajabu kuhusu hilo ka zako bado hazijafika utarudi tuu,binafsi nimewahi kutokewa na kisa ka hicho,number yako ikiwa haijafika basi utarudishwa duniani,hivyo ndio mwenyezi mungu anavyofanya kazi.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!