Duka
la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba
moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
Moto ukiwa unazidi
Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia tutuki la Moto
Kazi za uokoaji zikiwa zimeanza huku wasamalia wema wakisaidia kuhamisha vitu
Maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto kwa kasi
Baadhi ya vyombo na vifaa vya duka la kushonea nguo vikiwa vimeokolewa
Kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea
Moshi Mkubwa uliowachanganya watu na kila mmoja kuanza kutaka kukimbia eneo la tukio
Vijana
wasamalia wema wakiwa wameacha kazi zao za kutengeneza magari, kufyatua
matofari na mambo mengine wakiwa wanafanya kazi ya kuanza kuuzima moto.
Vijana wakiwa wameanza kufanya kazi ya kuzima moto baada ya Kikosi cha zima moto kuendelea kuchelewa kufika
Maduka yakizidi kwisha kwa kuteketea kwa moto, Huku wananchi wakipata tukio moja kwa moja
Baadhi ya Vijana wasamalia mwema wakiwa wanaondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi
Sehemu ya nyaya za umeme uliosababisha moto huo.
Upande mwengine wa mashuhuda
Vijana wakiwa bize wanafanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano
Vijana wakiwa wanashughulika kwa nguvu zote ili wapate kuzima moto mara moja
Kikosi
cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi
wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyo ungua
Mabaki ya vitu katika duka la vitambaa ya nguo na ushonaji
Wananchi wa mwananyamala wakiwa wanasikika wakisema "Wamekuja zima moshi... wamekuja zima moshi..."
Kazi
ikiwa imeisha hizi ndizo ndoo ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa
kuzima moto pamoja na baadhi ya vijana wachache walio saidia kuzima moto
huo.
*******
Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme umewaka eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.
Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme umewaka eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.
Moto
huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio
waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae
Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea
kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.
Katika
tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhuriwa ingawa katima maduka
yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia
kuteketea vibaya kwa moto huo.
No comments:
Post a Comment