Muonekano wa karibu zaidi wa shimo hilo.
SIKU chache baada ya kukutwa mauzauza katika kaburi la mwigizaji Rachel Haule ‘Recho’, kaburi la mwigizaji Adam Kuambiana (pichani)limekutwa limetoboka kimaajabu.
Gazeti la Risasi Jumamosi toleo la Julai 19, mwaka huu lilikuwa na babari yenye kichwa cha habari kisemacho: ‘Uchawi kaburini kwa Recho.’ Kwenye habari hiyo, ilielezwa kuwa katika kaburi la Recho kulikutwa tunguri iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.
Baada ya habari hiyo, siku mbili baadaye, chanzo kingine kiliwapigia simu waandishi wetu na kuwaeleza kuwa mbali na tukio la Recho, kaburi la Kuambiana limetoboka kimaajabu na kuzua mtafaruku miongoni mwa watu walioshuhudia kwa mara ya kwanza tukio hilo.
“Jamani haya ni mambo ya kishirikina, huwezi amini kaburi hili limetoboka ghafla kimaajabu maana juzi tu nilikuja kutembelea makaburi haya, lilikuwa halijatoboka,” kilisema chanzo hicho.
Mapaparazi wetu walifika katika makaburi hayo na kujionea kaburi hilo likiwa limetoboka huku watu wengi waliokuwepo eneo hilo walidai kuwa tukio hilo si la kawaida kwani limetokea wakati ambao mvua hazijanyesha
No comments:
Post a Comment