Hongera sana Mr. President ‘Jakaya M. KIKWETE’
“I am
Moved”, sababu nikirudi nyuma kidogo katika historia ya nchi ya Tanzania
mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati sanaa ya muziki wa kizazi kipya
ilipoanza kuchipuka ikifuatiwa na vita kubwa dhidi ya kukemea kijana
kuwa msanii waHIP HOP nchini na sanaa hii kupewa majina ya kutisha kama
muziki wa “kufoka foka, kihuni”na sanaa hii haikukubalika kabisa katika
jamii ya kitanzania.
Binafsi
naweza nikasema kipindi cha awamu ya 4 ya uongozi wa serikali ya
Tanzania kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete’ ndio wakati pekee ambapo wasanii na sanaa ya kitanzania
inaweza kujivunia sana. Kwanza kabisa naweza kudiliki kusema ndio wakati
pekee wasanii wa nchini wameweza kutembelea IKULU ya Tanzania kuliko
vipindi vyote vilivyopita na pia kuwa ni kiongozi ambae amekua na
ukaribu wa hali ya juu na wasanii wa nchini. Hata mimi binafsi ambae
sijawahi kupata nafasi ya kuingia IKULU, natamani ningekua msanii
kipindi hichi ili niweze kupata nafasi ya kuwa na ukaribu na Rais wa
nchi yangu na naamini inaleta msukumo mkubwa sana kwa vijana ambao
wanafanya sanaa nchini Tanzania kwa sasa.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kuanza tu naweza nikasema dhana ya upendo wa sanaa
hii ya Tanzania hajaanza nayo jana wala juzi, sababu kipindi cha nyuma
wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikuwa
mstari wa mbele kusikiliza sana muziki wa bongo na alikua anahakikisha
anakwenda nao kwa jinsi unavyozidi kukua.
Rais Kikwete
sehemu yake kubwa nakumbuka alikua anahakikisha anapata nyimbo mpya za
bongoflava zikitoka ilikuwa ni katika kituo cha Radio cha Clouds FM
wakati huo ofisi za radio hiyo zilikuwa pale katika jengo la Kitega
Uchumi Samora Avenue. Juhudi za kiongozi huyu wa ngazi ya juu kabisa
nchini hazijaishia hapo hata baada ya kuingia madarakani bado tunaziona
kwa mialiko kadha wa kadha anayoitoa kwa wasanii kuweza kuingia Ikulu na
kupata nao chakula, pia kuzungumza nao na kuwasikiliza matatizo yao ya
kimaisha pamoja na kisanii. ukiwa kiongozi wa ngazi za juu katika nchi
yoyote majukumu yako ni makubwa sana na ni ngumu kutatua matatizo ya
kila mwananchi na kila sekta lakini kuweza kutafuta muda wa kuweza
kukutana kuongea nao na kuwasikiliza tu ni kitu mabacho hakijawahi
kitokea kwa viogozi wote wa kiserikali waliopita.
Si hapo tu
Mheshimiwa Rais ameweza kutumia nguvu na juhudi zake kuweza kuwaletea
wasanii studio inayoeleweka nchini ili waweze kutengeneza muziki na
audio recording zenye viwango vya kimataifa pamoja na malalamiko ya hapa
na pale kuwa studio hiyo haijulikani ilipo na inafanya nini hivi sasa
lakini hayo sio makosa yake na sidhani kama yanamuhusu, mheshimiwa
ameweza kuwapatia kitu hicho na ameendelea na harakati zake kusaidia
sanaa hivyo, sitegemei yeye ndio akae kusimamia kuendesha shughuli hiyo
wakati ana mambo lukuki na matatizo ya wananchi wengine ya kutatua.
Mbali na
hiyo tumeona msaada wake binafsi ambao aliutoa kuweza kumsaidia msanii
Ray Cee ambae alikua ameharibikiwa kwa utumiaji wa madawa ya kulevya,
aliweza kumsaidia na hivi sasa amerudi katika hali salama na kuweza
kuendelea kufanya harakati zake za kisanii na kusaidia vijana wengine
kuondokana na utumiaji wa madawa ya kulevya katika Foundation yake
ijulikanayo kama Ray C Foundation.
Juzi tu
akiwa nchini Marekani, tumeona alifanikiwa kumkutanisha msanii Diamond
Platnumz na mtaalam wa ngazi ya Juu wa muziki wa nchini Marekani ambae
anasimamia wasanii kama “Trey Songz na Big Sean ajulikanae kwa jina “Mr
Kevin Liles”, huko Manhattan New York City ili aweze kumsaidia msanii
huyo ambae amefika hadhi ya kimataifa na kuweza kuwa nominated kwenye
tuzo kubwa sana za muziki Duniani kama MTV pamoja na BET na wasanii
wengine wa Tanzania ambao wanachipukia katika tasnia ya muziki.
Rais Kikwete
hakuishia hapo, aliahidi kuleta na kusaidia tasnia ya muziki na Filamu
nchini na amedhihirisha wazi kuwa hajachoka kwa kuweza kufanikisha
kuleta wasanii wakubwa sana toka nchini Marekani ambao wapo nchini
Tanzania kwa sasa ambao wanafanya Workshop inayoendela katika kumbi za
Bank Of Tanzania hivi sasa kwa ajili ya wasanii nchini kupata elimu
zaidi ya kazi zao kisanii wanazofanya. Mheshimiwa Rais amefanikiwa
kuwaleta Hip Hop Legend Rapper/Producer/Actor/ DAVID BANNER msanii toka
MISSISSIPI USA ambae ameshaweka historia kubwa sana katika tasnia ya
filamu pamoja na muziki wa Hip Hop ambae yupo nchini pamoja na TERRENCE J
ambae alikuwa mtangazaji wa TV kwenye kipindi maarufu sana ndani ya BET
ambapo nafasi yake imechukuliwa na msanii aliebadilisha jina lake hivi
karibuni kwa mara ya pili kutoka Lil’ BOW BOW alilopatiwa na msaniiSNOOP
DOGG wakati akiwa mdogo na kwenda BOW BOW alipokuwa mkubwa na juzi tu
amebadilisha tena na anajulikana kwa jina lake halisi SHAD MOSS ambae
anafanya kipindi kijulikanacho kama 106 & PARK. TERRENCE J ambae kwa
sasa ameingia kwenye tasnia ya Filamu na kushiriki filamu ambayo ni
maarufu sana na mastaa wengi nchini marekani “THINK LIKE A MAN TOO”
ambayo inaangaliwa sana na ipo katika cinema duniani kwa sasa,
iliyotokana na kitabu kilichoandikwa na Legendary comedian“STEVE HARVEY”
na hii ni filamu ya 2 kutoka ambayo inetengenezwa kutokana na kitabu
hicho.
Sanaa ni
kitu ambacho huingizia kipato kikubwa sana cha kodi katika serikali za
nchi zilizoendelea kutokana na usimamizi mzuri ambao serikali za nchi
hizo zimeweza kutengeneza mfumo wa kuweza kuwalinda wasanii pamoja
kusimamia haki za kazi zao, vile vile hutengeneza ajira nyingi sana kwa
vijana wenye vipaji vya sanaa kuweza kutumia sanaa hiyo kujitengenezea
maisha zaidi ya kusubiri mpaka wakaajiriwe.
Sanaa hii ya msanii mmoja
kwa mfano kama ALIKIBA, OMMY DIMPOZ, DIAMOND Platnumz au LADY JAY DEE
ambao wana mafanikio makubwa sana katika tasnia ya muziki wa kizazi
kipya nchini, wameweza kusababisha vijana wengi kupata ajira kama wale
wanaocheza kwenye show zao (Dancers), watengeneza muziki wao
(Producers), wasimamizi wa kazi zao (Managers), mtengeneza Video (Video
Director) na wengine wengi, ambapo swala la ajira tunalijua lilivyokuwa
gumu nchini na duniani kwa ujumla.
Tunaelewa
kabisa kuwa kiongozi wetu huyu amebakiza muda mfupi sana madarakani
lakini kwa nguvu hii ambayo ameionyesha mpaka sasa sidhani kama ataishia
hapo hata kama akiwa hayupo madarakani. Namuombea heri na afya njema
aweze kuendeleza mchakato huu ambao ameufanya mpaka sasa katika sanaa ya
Tanzania, mungu ampe nguvu asichoke sababu naamimi wasanii wote nchini
tupo nyuma yake kuendeleza legacy ambayo ameianza, vile vile viongozi
wengine na kiongozi wa nchi anaekuja baada ya yeye aweze kusaidia
kufungua milango na kumsaidia zaidi Baba wa Wasanii nchini Dk JAKAYA
MRISHO KIKWETE kwa moyo wake na msukumo wa kusaidia sanaa nchini
alioanza nayo zaidi ya miaka 10 iliyopita na mimi binafsi nikiwa kama
shahidi kwa makubwa aliyoyafanya mpaka hivi sasa.
Hongera
mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete’ kwa kazi yako nzuri ya kusaidia sanaa nchini Tanzania na Mungu
akubariki sana.
By: GongaCEO
CHANZO ANKAL MICHUZI
No comments:
Post a Comment