
BALOZI wa Ufaransa nchini, Marcel Escure, ameahidi nchi yake itashirikiana kwa karibu na Wizara ya Maliasili na Utalii kulifanya eneo la Mapango ya Amboni, mkoani Tanga kuwa maalumu la utalii na lenye kuvutia.
Balozi Escure alitoa kauli hiyo mkoani hapa juzi alipotembelea na kufanya utalii kwenye mapango hayo yenye kilometa za mraba 234, yaliyoko Kata ya Kiomoi, Tarafa ya Chumbageni, Wilaya na Mkoa wa Tanga.
Balozi huyo aliyekuwa ameambatana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alionyesha kushangazwa na namna mapango hayo yenye miamba mingi yenye maumbo ya kuvutia kama meli, mamba, na mchoro wa chui.
Waziri Nyalandu alisema licha ya kulitangaza na kulifanya eneo hilo kuwa maalumu kwa utalii, ataandaa mpango mkakati wa kuliboresha sanjari na kuruhusu wanyama wapole wahifadhiwe katika mapango hayo, ili kuongeza utalii.
Hata hivyo, Nyalandu amepinga kuingizwa umeme ndani ya mapango hayo, ili kuruhusu matumizi ya taa na badala yake alisema ataandaa mpango wa kutengenezwa tochi maalumu.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale, Donatius Kamamba, alimueleza Waziri Nyalandu kuwa eneo la hifadhi ya mapango hayo yaliyokuwa chini ya maji ya bahari miaka milioni 20 iliyopita, linakabiliwa na changamoto ya maji yanayojaa kutoka kwenye mto unaopita kando ya mapango hayo, hivyo kusababisha uharibifu wa ardhi
No comments:
Post a Comment