Kesi inayomkabili Amina Maige kwa kosa la kumng'ata na kumchoma kwa pasi mfanyakazi wake wa ndani Yusta Lucus miaka ishiriani haikuweza kusikilizwa na mahakama ya kinondoni baada ya mtuhumiwa kutofika mahakamani hapo.
Kesi hiyo inayomkabili Bi Amina Maige imeshindwa kuoendelea kama ilivyopangwa licha ya mashahidi wawili pamoja na mwathirika wa tukio hilo kufika mahakamani hapo kwa madai kuwa mshtakiwa mgonjwa ambapo wadhamini wa mtuhumiwa walihudhuria makahamani hapo.
Hakimu mkazi Flora Mtarania ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 13 Agusti mwaka huu.
Wakati huo huo kesi ya wizi wa mamilioni ya shilingi katika benki ya Barclays inayowakabili washtakiwa 12 wakiwemo washtakiwa wawili wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Mtawa wa kanisa katoliki imetajwa katika mahakama ya kisutu jijini Dar es salaam.
Washatakiwa hao wamepandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu Nyigulila Mwaseba wakituhumiwa kwa kesi ya unyang`anyi wa kutumia silaha na wizi wa shilingi milioni mia tatu tisini nukta mbili,dola 55 elfu za kimarekani na yuro elfu mbili mia moja na hamsini katika bank ya Barclays tawi la kinondoni ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi August 05,mwaka
No comments:
Post a Comment