Tuesday 22 July 2014

ALEX MASSAWE AWATOROKA POLISI.

  Mfanyabiashara, Alex Massawe anayesakwa kwa kesi ya mauaji.
UONGOZZI mpya wa Jeshi la Polisi Tanzania chini ya IGP Ernest Mangu umesema unafuatilia kwa karibu nyendo za mfanyabiashara, Alex Massawe ili akamatwe na kumrejesha Bongo kukabiliana na kesi ya mauaji inayomkabili yeye na mfanyabishara mwingine, Marijani Abubakar Msofe ‘Papa Msofe’.


arifa kutoka vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo zinadai kwamba, viongozi wa juu wa polisi walisema Massawe alifuatiliwa kwa karibu na Jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol) akiwa Dubai lakini alipogundua yuko mtegoni alitoroka na kwenda Afrika Kusini ambako anaishi hadi sasa. 

Chanzo kikasema kuwa, IGP Mangu amesema haoni sababu ya mfanyabiashara huyo kukamatwa na kuletwa nchini kuwe ni hadithi ya muda mrefu wakati uwezo wa kumnasa upo.
Massawe anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi, Novemba 6, 2011 nyumbani kwake Magomeni jijini Dar es Salaam. 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ilitoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini kwa Massawe ili kukabiliana na kesi mbili ikiwemo ya kughushi nyaraka mbalimbali.

Alex Massawe (kulia) wakati akiwa nchini.
 Massawe anakabiliwa na kesi hiyo ya mauaji namba 150/2013 ambapo mtuhumiwa wa kwanza Papaa Msofe na mwenzake Makongoro Joseph Nyerere wapo Gereza la Keko, Dar wakisubiri kesi hiyo.

Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita lilimtafuta IGP Mangu kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hili ambapo alisema Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCI)  anaweza kusema yote.

Mfanyabishara Marijani Abubakar Msofe ‘Papa Msofe’ akiwa chini ya ulinzi.
 Uwazi likamtafuta DCI Isaya Mngulu ofisini kwake, Dar na alipoulizwa juu ya suala hilo alisema ofisi yake kwa kushirikiana na Interpol linamsaka kwa udi na uvumba mtuhumiwa huyo.
“Ni kweli tunamtafuta Massawe, naamini  tutamkamata muda si mrefu na kurejeshwa nchini kukabiliana na kesi yake. 
 “Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa amewahi kukamatwa Dubai, hiyo si kweli. Inasemekana alikuwa huko na aliposikia anatafutwa akakimbilia Afrika Kusini, tutamkamata tu,” alisema DCI Mngulu.


CRD:GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!