Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamekataa
makubaliano ya kusitsisha vita na kutaka taifa hilo
ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
Afisa mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la Seleka ameiambia BBC kwamba wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo yalioafikiwa siku ya jumatano kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.
Mapigano ya miezi kadhaa kati ya makundi ya Wakristo na yale ya Waislamu katika taifa hilo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni wakiwachwa bila makao.Joseph Zoundeiko amewalaumu Wakristo wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa kuleta amani na kusema kuwa taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
lakini kundi la Human Rights Watch linasema kuwa wapiganaji hao wameelekea katika maeneo ya mashambani na kwamba wameanza kuzishambulia jamii za Wakristo.
Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili
No comments:
Post a Comment