Monday 26 May 2014

WANAHARAKATI WALAANI WANAWAKE KUUAWA KIKATILI

MTANDAO wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (Mkuki), umelaani matukio ya wanawake kuuawa kikatili na watu wasiojulikana ambao wakati mwingine huwakata na kuchukua viungo kwenye miili yao, ili kuvitumia kwenye masuala ya kishirikina hususan kutafuta utajiri.

Mkurugenzi wa WILDAF, Judith Odunga kwa niaba ya Mkuki, mtandao huo ambao unajumuisha mashirika 22, umeeleza kusikitishwa na kufedheheshwa na matukio hayo.
Kwa mujibu wa Odunga, mtandao wa Mkuki unatoa wito kwa jamii ya Watanzania wakiwemo viongozi wa jadi, viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji na wananchi kwa ujumla kubaini na kutovumilia ukatili huo na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya vitendo hivyo.
“Wito huu ni pamoja na kuwaomba wanajamii kuendelea kutoa taarifa za uwepo wa matukio haya kabla hayajatokea, kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tunaweza kuzuia kwa kiwango kikubwa badala ya kusubiri kutoa taarifa wakati uhai wa mama na dada zetu ukiwa umeshapotea,” alisema.
Alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali, mtandao huo unatoa wito kwa serikali kuchukua hatua kali zaidi, ili kukomesha vitendo hivvyo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!