Monday 26 May 2014

WALIOITWA KWENYE INTERVIEW SERIKALINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



File:Coat of arms of Tanzania.svg

OFISI YA RAIS



SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/22 24 Mei, 2014
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Wizara ya Maliasili na Utalii, MDAs & LGAs na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFSA), anatarajia kuendesha usaili na hatimaye

kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa 1:00 kabla ya muda wa mtihani
wa mchujo kuanza.
2. Kwa wale wasiokuwa na mtihani wa mchujo usaili utaanza saa
moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe kama
inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho
cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
4. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha
nne, sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”,
hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI
RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).

7. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa
usaili
9. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth
Certificate)
10. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba
tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
12. Kada zenye mchujo, wasailiwa watakaofaulu mtihani wa mchujo
wazingatie mahali na tarehe za usaili wa mahojiano kama
ilivyooneshwa kwenye tangazo.

DOWNLOAD MAJINA HAPA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!