Monday, 5 May 2014
VITUO VYA MAFUTA KUFUNGWA MASHINE ZA UTOAJI RISITI (EFDs.)
BAADA ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha matumizi ya mashine za kielektroniki za utoaji wa risiti (EFDs) kwa wafanyabiashara ndogo na wa kati, sasa imevigeukia vituo vya mafuta kwa kuwaanzishia utaratibu wa kufunga mashine za kielektroniki za utoaji wa risiti kwenye pampu zake.
Tayari muda wa mwisho kutekeleza agizo hilo umefikia Aprili 30 mwaka huu na kuanzia Mei Mosi vituo vyote nchini vimetakiwa kufunga mashine hizo ambapo kila pampu itakapomaliza kutoa mafuta hapohapo itatoka risiti kwa mteja inayoonesha kiwango cha mafuta kilichouzwa na gharama zake.
Akizungumza kwenye mafunzo kwa wanachama wa Mtandao wa waandishi wa habari za kodi Tanzania (TAWNET) jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema walivipa barua vituo vyote vya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini kuhusu suala hilo.
“Mfumo wa kutumia mashine za kodi za kielektroniki ulianza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza mwaka 2010 kwa wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na awamu ya pili ulianza mwaka 2013 ikiwahusu wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa kwenye VAT na wenye mauzo ghafi kwa mwaka ya Sh milioni 14 na zaidi. Lengo ni kusajili wafanyabiashara 200,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment