MAMA mmoja yeye huamka saa kumi na moja asubuhi, akoke moto,akande unga na kisha atengeneze chapati zakuuza. Hii ni kazi yake ya kila siku. Anti huyuamekuwa akipika chapati kwamiaka mitano sasa.
Anaziuza hivyo hivyo kwashida, maana kinachofuatia hapo ni kusubiri wateja, chapatimoja TSH 200/=. Bahati, hapo jirani yake akahamia mdada mmoja, akawa mteja wake, anachukua chapati mbili kila siku anaenda nazo kazini.
Mara yule mdada akaanza chukua nne,mara 8 mara 10, mara akaweka oda ya chapati 100 kila siku. Mama akawa hana jasho lakuuza tena, yaani dada wa watu akifika tu analamba chapati 100 anasepa. Kwa vile anachukua 100, mdada akaomba awe anauziwa moja kwa 150/=, anti akaona inalipa, anti akakubali, mdada sasa akawa anachukua chapati 200 kila siku.
Mamawa watu akaanza fuatilia kisirisiri, mdada anapeleka wapi?Kumbe yule dada anazichukua, anaenda nunua foil, anazifunga kwenye foil anauza Ofisini kwao na ofisi ya shosti yake jirani. Anauza moja Mia Tano. Mama kugundua, kaanza vimba, mara ananuna nuna, mara siku nyingine atengeneze 40 tu, mara aseme leo naumwa, mara leo nnaoda kubwa dadaangu siwezi kukupa, basi akendelea hivyo ili mdada ashindwe
Mdada akamwambia anti naona mie niache tu. Anti akafurahi. Keshoyake anti akatengeneza 200 akamtuma mtotowake wa kike akaziuze katika zile ofisi mbili, unajua nini, aliuza 10 tu.
Yule mdada alishaangaliaga plan B, anachukua kwa mama mwingine, tena anazipata kwa mia mia, sasa ana ofisi ya 3 anasaplai chapati 300 kila asubuhi. Kwa huyu mama mwingine jiko halikuwa zuri akampa jiko zuri na hotpots.
TUJIFUNZEE HAYA
1. Ukiuza Simu yako laki, aliyenunua akaendauza milioni, piga kimya,haikuhusu!
2. Ukiona mwenzako kafanikiwa kwa kufanya kitufulani, usidhanie basi nawe unaweza kufanikiwa kwa kitu kilekile kama yeye hujui nini siri ya mafanikio
3.Jifunze kutokana na mafanikio ya mwenzako sio kukasirika nakuweka bifu
4.Dada alishuhudia mwenzake akitumia foilkuweka chapati na kuuza ofisini yaani inavutia kununua kutokana na vifaavinavyotumika so ilibidi nae abadilike na kuwa kidijitali zaidi..
No comments:
Post a Comment