Saturday 24 May 2014

MKUU WA TUME YA UCHAGUZI WA MALAWI ATENGUA AMRI YA RAIS BANDA YA KUFUTA MATOKEO YA URAIS



Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Justice Mbendera amekaidi Amri ya Rais Banda ya kufuta matokeo ya uchaguzi. Mbendera amewaagiza maofisa wa tume ya uchaguzi kuendelea na zoezi la kuhesabu kura na kuomba ushirikiano wao wa dhati katika kipindi hiki kigumu.




Dakika chache Zilizopita,Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Malawi Justice Mbendera amekaidi Amri ya Rais Banda ya kufuta matokeo ya uchaguzi. Mbendera amewaagiza maofisa wa tume ya uchaguzi kuendelea na zoezi la kuhesabu kura na kuomba ushirikiano wao wa dhati katika kipindi hiki kigumu.

Amesema Rais hana mamlaka ya kuingilia tume ya uchaguzi ambayo inafanya kazi kikatiba na kisheria. Pia Rais Wa chama cha wanasheria wa Malawi (MLS) na Pia Mwanasheria Mkuu wa Zamani wa Malawi wameongea na Vyombo vya Habari Mud Mfupi uliopita na kusema ibara aliyoitaja Rais haimpi mamlaka ya kufuta uchaguzi..
Wamesema kifungu cha 5 cha sheria ya uchaguzi wa Bunge na Rais kinaipa Mamlaka Jukumu lote tume ya uchaguzi kusimamia mchakato wa Uchaguzi. Pia kifungu cha 100 cha sheria hiyo kinatoa haki ya chama au mgombea kulalamika kwa tume kuhusu ukiukwaji wa Mwenendo wa Uchaguzi na kama ndani ya masaa 48 hali hiyo isiporekebishwa kwa kiwango cha kuridhishwa basi kifungu namba 113 cha sheria hiyo hiyo kitatumika kupeleka mashtaka Mahakama Kuu.
Hata hivyo Mwanasheria mkuu akizungumzia Amri hiyo ya Rais leo hii amesema "Kuna Mtu anafanya uhaini hapa sasa" na kuendelea kudai kuwa Rais amefanya uhaini kwa kukiuka ibara ya 88 ya katiba ya nchi kutoa "Presidential Decree" bila sababu yoyote ya msingi inayozingatia katiba na mamlaka ya kisheria 


CRD: JMF

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!