Saturday, 24 May 2014

MAHINDI YENYE UWEZO WA KUMKUZA MTOTO KIAKILI


File:Klip kukuruza uzgojen u Međimurju (Croatia).JPG
Upo uhusiano mkubwa kati ya chakula atumiacho mtu kwenye enzi zake za utoto na ukuaji wake wa akili.
Uwezo wa akili wa mtoto hujidhihirishwa katika viwango vya kufikiria na kuchanganua mambo anapoanza kusoma darasani.

Hii inatokana na kanuni za kisayansi kwamba afya bora tangu utotoni humjenga mtu kiakili na kimaumbile. Hii ni pamoja na lishe bora na afya njema. Hata hivyo, wanasayansi wanasema lishe bora tu haitoshi kwa sababu suala la mazingira nalo huchangia katika kumjenga mtu.
Mazingira mabaya kiakili ni kama vile vita, malezi mabaya ya kifamilia, kukulia katika makundi maalumu kama vile makambi ya wakimbizi, vituo vya kulelea watoto yatima, elimu ya kiwango cha chini darasani na mtoto kujiingiza katika makundi ya vijana watukutu.
Pamoja na hali hiyo, wataalamu hao wanaamini kuwa matatizo ya mazingira yaweza kurekebishwa, lakini yale yanayotokana na lishe duni yanazaa tatizo la kudumu kimaisha.
Vyakula vyenye lishe bora ni vile vyenye mchanganyiko wa vyakula kama vile wanga, mafuta, protini, vitamini na chumvi chumvi.
Utafiti uliofanyika nchini unaonyesha kuwa familia maskini ndizo zinazoshindwa kupata vyakula bora. Katika uchunguzi huo inabainishwa kuwa familia nyingi hushindwa kutumia protini kutokana na gharama yake sokoni kuwa kubwa kama vile nyama, samaki na mazao ya jamii ya kunde.
Ni kutokana na utafiti huo, kampuni ya mbegu Tanzania, TANSEED iliamua kubuni mbegu za mahindi zenye kiwango kikubwa cha protini. Mtafiti wa TANSEED, Isaka Mashauri anasema waliamua kubuni mbegu hiyo kwa zao la mahindi kwa sababu ndilo linalolimwa kwa wingi zaidi nchini.
“Kilimo cha mahindi ni asilimia 80 ya mazao mengine ya chakula. Hili hutumika kwa wingi zaidi na hupatikana kirahisi zaidi,” anasema Mashauri ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa TANSEED.
Anasema aina hiyo ya mbegu ya mahindi waliyoipa jina TAN H611, tayari imeanza kusambazwa nchini.
Namna yalivyotengenezwa
Mashauri anatetea aina hii ya mahindi haikutokana na teknolojia ya Uhandisi Jeni, GMO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!