Monday, 5 May 2014

KIKWETE AKEMEA WANAOAMBUKIZA VVU

Rais Jakaya Kikwete amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na Serikali katika kampeni ya kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini.
Akizindua kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha Sh 1.5 bilioni zitakazotumika kusaidia kutokemeza maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi, Rais Kikwete alisema Ukimwi bado ni tishio.
Rais Kikwete alisema licha ya kwamba maambukizi mapya yamepungua kwa asilimia kadhaa ikilinganishwa na miaka iliyopita, bado jitihada zinahitajika kupambana na ugonjwa huo.
“Lengo la Serikali ni kukomesha maambukizi ya virusi vya Ukimwi, ingawa peke yetu hatuwezi, hivyo tunahitaji ushirikiano wa hali na mali kutoka taasisi nyingine za binafsi ili kufanikisha kampeni hii,” alisema Rais Kikwete.
Katika kampeni hiyo, Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM), inatarajia kukusanya Sh1.5 bilioni zitakazosambazwa mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kusaidia kupunguza maambukizi mapya.
Mwenyekiti mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho alisema zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro litafanyika kwa siku sita kuanzia Mei 15 na washiriki wataanza kuwasili mjini Moshi Mei 14.
Mrisho alisema lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wanapunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) hadi kufikia asilimia sifuri na kupunguza vifo vitokananyo na ugonjwa huo na kumaliza unyanyapaa kwa waathirika.
“Kampeni hii inafanyika mwaka wa 13 sasa. Mwaka jana tulikusanya milioni 700 katika kampeni kama hii. Fedha ambazo zimesaidia kupunguza mara mbili zaidi,” alisema. ya maambukizi mapya kulinganisha na miaka ya nyuma,” alisema Mrisho.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM, Michael Van Anen alisema kampeni hiyo itahusisha wananchi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Anen alisema katika kampeni hiyo watoto wawili wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Moyo wa huruma kilichopo Geita wataungana na wananchi wengine kupanda mlima Kilimanjaro siku hiyo.
“Tumefanikiwa kuzifikia na kuzisaidia asasi mbalimbali hapa nchini kupitia kampeni hii ambayo tumekuwa tukifanya na wadau wengine kama Captal Drill, Wambi Oil, Mantrac, Prime Fuel, African Barrick Gold, Airtel, Southern Sun, Zara, MACS, Ausdrill na wadau wengine wanaopenda kuungana kufanikisha kampeni hii pamoja na sisi.
“Tunafanya kampeni kwa lengo la kusaidia kupunguza ukimwi ambao kwa hapa nchi bado ni tishio,” alisema Anen
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!