Mwili wa mwanamuziki Amina Ngaluma ukipokelewa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ukitokea Thailand alipofia.
Waombolezaji wakiwemo waandishi wa habari wakisubiri mwili wa marehemu Uwanja wa Ndege wa J ulius Nyerere Dar.
Mume wa marehemu Amina, Rashid Sumuni ambaye pia ni mwanamuziki akiwa na huzuni uwanja wa ndege wakati anasubiri mwili wa mkewe.
Baba wa marehemu mzee Kassim Ngaluma ( mwenye kofia) akiwa na huzuni wakati anasubiri mwili wa marehemu.
Mwanamuziki Cosmasi Chidumule (Katikati) akijadili jambo na wadau wa muziki akiwemo Mzee Mbizo (kulia).
Mwanamuziki Mwijuma Muumini akihojiwa na mwanahabari kabla ya maiti haijafikishwa uwanja wa ndege Dar.
Waombolezaji wa msiba huo mmoja akilia kwa uchungu wakati wa kuupokea mwili wa Amina Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar.
Shemeji wa marehemu ambaye ameoa mdogo wake na Amina Ngaluma akisubiri kuwasili kwa maiti Uwanja wa Ndege wa JK Dar.
Hatimaye mwili wa aliyekuwa mwanamuziki wa muziki wa dansi nchini Amina Ngaluma umewasili jana usiku jijini Da ukitokea nchini Thailand.Mwili wa marehemu uliwasili kwa ndege ya K.L.M saa 4 kasoro robo usiku wa jana, huku baadhi ya wadau wa muziki na wanandugu wakionesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wanamuziki kutokufika katika kuupokea mwili wa Amina Ngaluma.
Kamera yetu ilishuhudia wasanii wachache waliowasili eneo la Uwanja wa Ndege akiwemo Mzee Cosmasi Chidumule na Mwijuma Muumini ambaye alitoka Kahama kwa ajili ya kuudhuria mazishi ya mwanamuziki huyo anayetarajiwa kuzikwa leo mchana.
(Picha zote Gabriel ng’osha na Harun Sanchawa/GPL
No comments:
Post a Comment