Monday, 5 May 2014

HABARI ZA UMBEYA........HII NI COPY N PASTE TOKA HUKOO!

BARUA YA WAZI KWA FAMILIA YA DIAMOND PLATNUMZ

 Sikufanikiwa kupata anwani ya familia ya Diamond nikawatumia barua hii kwa hiyo nikaona niwatumie kwa kupitia blog yetu. Nakumbuka siku za nyuma mlikuwa nyuma ya kijana wetu kwenye kila kitu ,hususani kwenye show zake. Ila toka arudiane na bibie Wema sijawaona mkiwa nae kwenye public hususan kwenye show zake.


Bi Sandra ulikuwa hukosi show za mwanao Diamond, ukiambatana na wanao Esma na Queen Darleen , ila siku hizi mpaka nimeanza kuisahau sura yako mama Diamond kwa jinsi ulivyopotoea. Nakumbuka mara ya mwisho kuwaona mkiwa na kijana wenu ilikuwa ni pale Serena hotel akiwa ana launch video yake ya Ngololo. Kwa kweli mlikuwa na furaha sana dada zake Esma na Queen Darleen walifanya na interview wakiwa na wifi yao Penny. Leo hii kijana wenu anapokea tuzo kubwa Tanzania nzima kwa huo huo wimbo wa Ngololo ila familia nzima hamjafika kutoa support, sisi kama washabiki wake tunajiuliza maswali mengi sana, je hamkufika sababu Diamond alienda na mpenzi wake wa sasa Wema Sepetu na sio Penny?
Kijana wenu alivunja rekodi siku ya jana kwa kupata tuzo nyingi zaidi ya msanini yoyote Yule lakini hamkuwepo kushuhudia tukio hilo yote hiyo ni sababu ameamua  kuwa na Wema ,sisi kama watanzania mnatusikitisha sana jinsi mnavyoshindwa kutoa support kwa Diamond na Wema. Dada zake walikuwaga ni hodari sana kutangaza show za kaka yao huko instagram lakini toka awe na Wema tunaona kimya ,hakuna anaetangaza show zake. Halima Kimwana (Ndugu wa kufosi) huwa hakosi kutangaza show za Diamond kwa kuweka poster kwenye instagram yake lakiniilei show ya Mtwara iliyofanyika siku chache zilizopita ndio show ya kwanza ya Diamond ambayo Halima hajaitangaza na yote hiyo ni sababu Sura ya Wema ilikuwepo kwenye poster. Sisi kama fans wa Diamond na Wema kwa kweli mnatufedhehesha sana.
Nyinyi kina Esma kumbukeni na nyie ni wanawake pia na mtakuja kuolewa na mtakuwa na wakwe zenu. Je mtapenda wakwe zenu wakiwasusa kama nyie mnavyomsusa Wema mpaka hamuendi kwenda kwenye show za kijana wenu? Hatusemi msiwe karibu na Penny,mimi kama mimi nimewapenda sana jinsi mlivyo na msimamo na mlivyoendelea kuwa karibu na Penny hata baada ya kutoswa na kaka yenu lakini pia kuwa karibu na Penny haimaanishi mumtenge Wema. Mengi tunayajua lakini tumekaa kimya, Esma kaka yako kakupangishia nyumba na furniture kila kitu kakuwekea matokeo yake ni nini? Umeenda kumchukua Penny unaishi nae kwenye hiyo nyumba,hivi hapo unadhani Wema kama mwanamke anajisikiaje kuona ex wa boyfriend wake anaishi kwenye nyumba aliyolipia boyfriend wake? Hamuoni kama mnaleta matatizo kwenye uhusiano wao? Kwani Penny hana kwao? Kuna ulazima gani wayeye kuishi kwenye hiyo nyumba na Esma?
Na siku Wema na Diamond wakizaa mtoto je mtawachukia watoto sababu ni wa Wema pia? Kumbukeni kwamba siku hazirudi nyuma na mnakosa sehemu kubwa sana ya maisha ya Diamond hususani kwenye career yake. Oneni sasa jana mmekosa kufurahi nae kama mlivyokuwa mnafanya huko nyuma, mmekosa kufanya yale ma interview mnayopenda kufanya nae eti kisa yuko na Wema. Haya sasa na birthday yake inakuja mwezi wa kumi ,mwaka jana mlikuwa nae akiwa na Penny mkatandika mashuka na maua kitandani mkapiga mapicha na mazagazaga kibao. Mwaka huu atakuwa na Wema Sepetu sasa mtakosa kula keki na kaka yenu sababu ya Wema?
Bi Sandra wewe ndo kichwa cha familia , tunakuomba ulifikirie hili na uiweke familia yako sawa. Sisi kama fans tumemiss sana kuwaona kwenye public mkila good time na Diamond. Tunaomba muelewane na Wema for the sake of Diamond, naamini Diamond angependa kuona familia yake ikiwa karibu na mwanamke anaempenda yeye.
Ni hayo tu kwa leo, yani jana roho iliniuma sana kumuona Diamond akiwa na ndugu mmoja tu karibu yake, Yule Rommy Jones na wakati wote tunajua familia ya Diamond ni wapenda shughuli yani kama angekuwa na Penny jana wasingekosa. Matokeo yake mmeishia kuweka vipicha viwili vya diamond akiwa na award zake huko Instagram mnamuwishi kinafki nafki.Lakini ya Mungu mengi Diamond alikuwa na furaha jana, Wema Sepetu na Rommy Jones walimliwaza sana.
Mie nawapa onyo tu kuwa kuweni makini msidhani mkifanya hivyo ndo Kaka yenu atamuacha Wema Sepetu, wale wanapendana, wana mapenzi ya ukweli mtu ukiwaangalia tu unaona jinsi walivyoshibana. Asije akamchagua Wema akawasahau nyie. Akisema awapotezee mtaishije wakati yeye ndo kula yenu na vaa yenu? Au Penny ataweza kuwalisha iwapo Diamond atachukia na kuwapotezea? Jiangalieni sana matendo yenu kwa Wema na jana  Wema kasema mbele ya kadamnasi yeye ni wife to be sasa na harusi mtasusia? Acheni chuki zisizo na kichwa wala miguu.
Naomba nimalizie kwa kusema kuwa jana mmetia aibu sana, hakuna hata mmoja wenu aliefika kwenye shughuli. Bi Sandra miaka ya nyuma ulikuwaga unapanda jukwaani na mwanao leo hii kaweka historia do hujatokea yote hayo kisa mwanamke anaelala na mwanao humtaki? Huu sio uungwana kabisa. Wewe Esma unavyokuwaga wa mbele mbele kwenye show za kaka yako jana umeshindwa kufika?Mpaka Halima Kimwana (Ndugu wa kufosi) kazizima, kimyaa. Kwanini mnakuwa hivi? Wema kakosa nini jamani? Tuelezeni watanzania. Kwa vyovyote vile lazima Diamond anaumia sana na Wema pia atakuwa anaumia ndani ya nafsi yake kuchukiwa hivi na familia ya mume wake mtarajiwa.
Nawapenda sana Wema na Diamond
Anoni.
CRD: U-TURN

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!