Wednesday 28 May 2014

DAR INASAMBAZA DENGUE MIKOANI



UGONJWA wa homa ya dengue umeanza kusambaa kwa kasi mikoani ambapo sasa wagonjwa wapya 50 wamegundulika huku ikielezwa wengi ni waliotoka nao mkoani Dar es Salaam. Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Afya na Dharura, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Elias Kessy.



Alikuwa akitoa taarifa kwa Naibu Wa- ziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe wakati wa kufunguliwa mafunzo kwa Waganga Wafawidhi wa Mikoa, Maofisa Afya, Wauguzi Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania yenye lengo la kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Alisema mpaka sasa wagonjwa wapya 50 wamegundulika katika mikoa kadhaa nchini ambapo asilimia kubwa ya watu hao wali- kuwa wamesafiri kutoka jijini Dar es Salaam na kuingia na ugonjwa huo kwenye mikoa waliyokwenda.

Alisema tangu ugonjwa huo uanze Januari mwaka huu zaidi ya watu 850 wameugua na wagonjwa wanne kati yao walipoteza maisha. Alisema jiti- hada zinaendelea kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Alisema bado tatizo hilo ni kubwa na utafiti unaendelea na Wizara kwa kushirikiana na Bohari Kuu ya Madawa (MSD), wamekuwa wakisambaza vifaa na dawa kwenye maeneo mengi nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya alisema ugonjwa huo ni mpya katika ukanda wa joto. Alisema ni muhimu kujipanga kuhakikisha ugonjwa huo hauenei kama ilivyo sasa.

Alisema kazi ni kubwa iliyofanyika katika kutibu wagon- jwa waliogundulika lakini jambo la muhimu ni kuangalia suala zima la usafi wa mazingira.
“Tumekubaliana kupita nchi nzima kuangalia suala la usafi wa mazingira linapewa kipaumbele, maeneo mengi yamekuwa na nyasi, madimbwi na hata matairi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa mazalia makubwa ya mbu kutokana na maji kutuama humo kwa muda mrefu,” alisema. 


Alitaka wataalamu hao wa afya kusimamia vizuri suala la usafi wa mazingira na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Tiba pekee ya homa ya dengue ni usafi wa mazingira, wataalamu kwenye halmashauri walione hilo, tatizo hili liko mbele yetu tukiligeuza kuwa malaria ya pili litakuwa tatizo kubwa sana,” alisema. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Ezekiel Mpuya alisema hospitali ya mkoa ilipata kesi moja ya mtu aliyeku- wa akiugua ugonjwa huo.

“Huyo aliyeugua alikuwa amekwenda Dar es Salaam kikazi na aliporudi akaanza kuumwa na kulazwa lakini alitibiwa na kupona na sasa hakuna mgonjwa tena hapa Dodoma,” alisema.


Washiriki zaidi ya 70 wanahudhuria mafunzo hayo. Ugonjwa huo unaotokana na kirusi kinachosambazwa na mbu aina ya Aedes , unatajwa kuwa ni wa ukanda wa joto. Dalili za ugonjwa huo ni homa, kuumwa kichwa, mau- mivu ya viungo na uchovu huku wakati mwingine, dalili zake zikifanana na za malaria.

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni bungeni, ilisema Sh milioni 132 zimeshatumika na wakati huo huo Sh milioni 540 zimetengwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa dengue ulioibuka jijini Dar es Salaam.

Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe katika taarifa yake bungeni, ilisema imeshafanya utafiti mkoani Kagera, Morogoro na Kigoma na kuthibitisha kuwa haijaathirika na ugonjwa huo. Dk Kebwe alisema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukabili ugonjwa huo kadri itakavyohitajika.

Alihimiza uvaaji wa nguo ndefu na zenye mikono mirefu hususani katika maeneo ambayo ugonjwa huu umeripotiwa kuepuka kuumwa na mbu husika.

HABARI LEO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!