Tuesday 27 May 2014

ATCL YATAKIWA KUJITANUA ZAIDI

Wafanyabiashara na wananchi mbalimbali nchini wameeleza kufurahishwa na taarifa ya kurejeshwa kwa huduma za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kati ya Arusha na Zanzibar.
Huduma za shirika hilo zilisitishwa kwa muda wa takriban miaka minne kutokana na matatizo kadhaa yaliyolikabili shirika hilo.
Huduma hizo sasa zimerejeshwa baada ya kuzinduliwa kwa usafiri huo mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Tumefurahi sana baada ya shirika kurudisha huduma zake. Itakuwa rahisi sasa kwa watalii na wafanyabiashara wanaosafiri kati ya maeneo haya mawili,” alisema Gladness Shoo, mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam na kuongeza:
“Mara nyingi napata wageni ambao hutaka kutembelea maeneo haya mawili kutokana na mvuto wa kitalii. Ilikuwa changamoto kupanga safari zao, lakini sasa nadhani dawa sahihi imepatikana”.
ATCL inatarajia kuwa na safari sita kwa wiki kati ya Arusha na Zanzibar jambo linaloonekana kuwa neema kwa wafanyabiashara, watalii na hata wafanyakazi ambao hutakiwa kuhudhuria vikao na semina mbalimbali zinazofanyika katika jiji la Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyesafiri na ndege ya shirika hilo kutoka Dar es Salaam mpaka Arusha alikaririwa na vyombo vya habari akisema shirika limedhamiria kuweka ushindani wa kweli katika sekta ya usafiri wa anga kwa kutoa huduma bora kwa bei nafuu. “Kusafiri na ATCL ni fahari sana. Unajisikia kuwa kweli wewe ni Mtanzania kwa sababu unasafiria shirika ambalo ni mali yako,” aliongeza Shoo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walishauri ATCL kwenda mbali zaidi kwa kuanzisha huduma imara za usafiri kama yalivyo mashiriki kama Kenya Airways la Kenya ambalo husafirisha abiria kwa masafa ya ndani na nje ya Kenya.
“Kenya wameweza, sisi Tanzania tunashindwa nini kuifanya ATCL kuwa imara?” alihoji Halima Mwanga, mkazi wa Mabibo
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!