Thursday 17 April 2014

WANAWAKE WATAKIWA KUWANIA UONGOZI MAJIMBONI

CHAMA cha Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) kimewakata wanawake wenzao kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali badala ya kusubiri nafasi za uteuzi.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Suzan Lyimo, alipokuwa atijibu hoja za wajumbe na wabunge katika semina ya jinsi ya kuchambua rasimu ya pili ya Katiba mpya.

Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo wanawake wakati wa kujadili rasimu hiyo na kutaka mapendekezo yao kuingizwa katika katiba.
“Pamoja na wanawake kutaka asilimia 50 kwa 50, lakini wanawake msipojitokeza kugombea majimbo ni wazi kuwa mtaendelea kukosa haki zenu.
“Mimi naona ni vema hata kama suala la ubunge wa viti maalumu ukisitishwa ili kina mama twende majimboni tukagombee kwani jimbo si mali ya wanaume. Kila mtu ana haki ya kugombea na kunadi sera zake,” alisema Lyimo.
Akizungumzia wanawake ambao tayari wana majimbo alisema ni wajibu wao kufanya kazi vizuri na wananchi ili waendelee kupata kibali.
Akijibu hoja ya Anne Kilango Malecela ambaye alitoa vitisho kuwa hataki mtu yeyote kugombea katika jimbo lake, alisema hata kama ni mwanamke haizuii mtu mwingine kugombea jimbo hilo kwani si mali ya mtu.
“Kwa mfano mwanamke ana jimbo, hiyo haizuii mtu mwingine kwenda kugombea kwa mfano kama wewe ni mbunge wa CCM na una jimbo, atakuja mgombea wa upinzani pia kugombea hapo, kinachotakiwa ni sera,” alisema

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!