Monday, 21 April 2014

TATIZO NI UAFRIKA WANGU TU! YAYA TOURE..


Manchester, England. Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure, mmoja wa wachezaji sita wanaowania tuzo ya mwaka huu Mwanasoka Bora wa Mwaka ya Chama cha Wanasoka wa Kulipwa wa England (PFA) wa England, amesema angekuwa na heshima kubwa duniani kama asingekuwa anatokea Afrika.


Kiungo huyo wa Ivory Coast anaamini yeye kama walivyokuwa nyota wengine wa Afrika kama Didier Drogba (Galatasaray) na Mcameroon, Samuel Eto’o (Chelsea) wangekuwa na heshima kubwa zaidi duniani, lakini asili yao ndiyo tatizo.
Nyota mwenzake wa City, Samir Nasri alisema mwezi uliopita kuwa ingekuwa habari nyingine kwa Toure kama angekuwa mzaliwa wa Ulaya au Amerika Kusini.
“Nafikiri alichosema Samir kina ukweli kabisa,” Toure aliiambia BBC. “Ukiwa mkweli kabisa mashabiki ndio wanaokufanya utambulike zaidi.
“Sitaki kuwa mkali na sitaki kuwa mtu wa kupinga, lakini nataka kusema ukweli.”
Toure ametwaa ubingwa wa ligi akiwa Ivory Coast, Ugiriki, Hispania na England na mwaka 2009 alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na Barcelona, lakini pamoja na mafanikio hayo bado hajulikani kama ilivyokuwa kwa nyota wa Barcelona, Lionel Messi au mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
“Kama utaenda sehemu yoyote Afrika watakwambia, tunamjua Messi, lakini unapokuja Ulaya na unaposema ‘Yaya Toure’ watu watakwambia, ‘ni nani huyo?’,” aliongeza.
“Baadhi watakwambia wanalijua jina langu, lakini hawaijui sura yangu. Lakini wanamjua Messi na sura yake. “Najivunia kuwa Mwafrika. Nataka kuwatetea watu wa Afrika na nataka kuionyesha dunia kuwa wachezaji wa Afrika wanaweza kucheza kwa kiwango cha juu sawa na wale wa Ulaya na Amerika Kusini,” alisema Toure.
Nyota huyo amefunga mabao 18 kwenye Ligi Kuu msimu huu na kuisaidia City kushika nafasi ya tatu.
, lakini ataukosa mchezo wa leo dhidi ya West Brom kutokana na kuumia

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!