Sunday, 13 April 2014
SOYA CHAKULA CHENYE KINGA NA TIBA
Mpendwa msomaji. Bado tupo katika kudadavua faida za kiafya zitokanazo na chakula.
Leo, tutaizungumzia Soya ambayo ni maarufu sana nchini lakini kwa bahati mbaya wengi
hawajui kuwa ni chakula chenye tiba ndani yake.
Ajabu ya chakula hiki ni pale kinapompa nguvu mgonjwa haraka bila kujali aina ya
ugonjwa anaoumwa. Katika ulimwengu wa vyakula, kuna maajabu mengi katika kukitumia
chakula kama tiba na kinga ya maradhi.
Mwaka 1999, Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini Marekani (UFDA),
iliwaruhusu wasindikaji wa vyakula kutangaza rasmi kuwa soya ni halali na sahihi kutumika
duniani kote kama tiba na kinga kwa maradhi ya moyo, yakiwemo shinikizo la damu, kiharusi n.k.
Kama vile haitoshi, taasisi nyingi za kupambana na kutibu maradhi ya saratani duniani zimekuwa zikihamasisha matumizi ya lishe ya soya kwa wagonjwa wa saratani za aina
mbalimbali baada ya kushuhudia nafuu wanayoipata wagonjwa kwa kutumia bidhaa za soya.
Lakini, wapo ambao ndoa zao zinalegalega kwa kukosa hamu ya ndoa. ‘Saponon’
ambayo imo katika soya ikitumika kwa wiki kadhaa tu hamu hurudi katika hali ya kawaida
kwa jinsia zote: wanaume na wanawake ‘Saponon’ huchachua homoni
zinazouchangamsha mwili na akili pia.
Ukiachana na faida hizo, zipo nyingine kama vile kutibu mzio (allergy) za aina zote,
hukarabati ngozi na hujaza madini ya ‘calcium’ na ‘boron’ kwenye mifupa na kutibu
maradhi ya maumivu ya viungo kwa wenye miili mikubwa, wajawazito na wazee pia.
Soya ina madhara yake pia isipotayarishwa ipasavyo. Soya ina chembechembe aina ya
‘purine’ ambazo zimejikita kwenye ngozi yake na zikiliwa, mwili wa binadamu huzigeuza
kuwa tindikali iitwayo ‘uric acids’ ambazo ndizo chanzo cha maradhi mengi yakiwemo ya
vifundo au ‘gout’, japo ‘uric acids’ hizo hutoka mwilini kupitia mkojo.
Ni vyema ikaeleweka kuwa kula mimea na nafaka ni sawa na kusafirisha madini kutoka
ardhini kwenda mwilini. Kitaalamu, unaweza usiipate soya bora kwa kuwa hutoka katika
aina tofauti za udongo wenye madini tofauti.
Hapo ningependa kukushauri kuwa kama kweli una nia ya dhati basi tumia soya iliyotoka
mikononi mwa wataalam ambao wameiandaa vema soya hiyo ikiwemo kuipitisha katika
mamlaka za udhibiti wa vyakula na madawa kama vile TBS na TFDA za hapa nchini
ambako huangalia kama hazina sumu zitokanazo na uchafuzi wa mazingira.
Soya inaweza kutumika kama kinywaji chepesi au kama uji au kwa kuchanganywa na
unga wa nafaka zingine na kutumika katika kuandaa vyakula vya iana mbalimbali
ukiwemo ugali. Hakikisha unapata unga wa soya ulioandaliwa vyema na kuutumia
utakavyo ili kuupa mwili wako kinga au kujipa nafuu ya haraka kama ni mgonjwa.
Tiba za vyakula ni nyingi kama tunavyoziona kupitia safu hii msomaji wangu. Nakuomba
usikose kila Jumanne kufuatilia makala haya ili tujikomboe kiafya kupitia milo sahihi
ambayo ndiyo tiba popote duniani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment