Thursday, 3 April 2014

MTI WA MWEMBE NI TIBA KUANZIA MAJANI HADI MIZIZI

TUNDA la embe linafahamika kutokana na kuwa na walaji wengi, lakini pamoja na kuliwa, lina kazi nyingi katika mwili wa binadamu.
Mbali ya kuwa ni tunda na juisi yake kuwa kiburudisho, mti wake una kazi nyingi zaidi ya unavyojua.

Mganga wa tiba asili, Abdallah Mandai, katika mahojiano na mwandishi wa makala hii, anasema mwembe kuanzia majani yake hadi mizizi ni tiba kwa binadamu.
Majani
Akianza na majani, Mandai anasema majani machanga yakichemshwa ni dawa ya pumu na pia huondoa matatizo ya kifua kikavu na kilichoiva.
Mandai anasema majani hayo pia hutumika kuoshea vidonda vya nje ya mwili ambapo hata kama mtu amepata ajali, huvikausha mara moja.
Unga wa majani hayo unaelezwa kusaidia katika kutunza meno ambapo mhusika atatakiwa kusukutulia na hivyo kuyafanya meno yake kuwa na nguvu wakati wote na kuepuka kuliwa na wadudu.
Kokwa
Wakati watu wengi wakiwa wanatupa kokwa kila wanapomaliza kula tunda hilo, Mandai anasema unga wa mbegu la mti huo ukinywewa mara 3 kwa siku ni dawa ya kuzuia kuharisha na kuhara damu.
Tunda
Watu wengi wakiwa wanapenda kula tunda hilo, ukweli ni kwamba hawajui kama wanajitibu minyoo na kuzuia uvujaji ovyo wa damu.
Akifafanua kuhusu minyoo ambayo watu wengi hudai inapatikana katika tunda hilo, hasa kwenye msimu wake, Mandai anasema inatokea hivyo kama mlaji atakuwa hajaliosha vizuri.
Hata hivyo, anasema kutokana na kuwa na madini ya vitamin C, husaidia kuponesha vidonda kwa haraka, na hivyo mlaji sana wa tunda hili endapo atapata majeraha basi atapona haraka kuliko yule ambaye hali kabisa.
Kwa wale wenye matatizo ya kupata choo, tunda hili linaelezwa kuwa tiba sahihi, ambapo kambakamba zinazopatikana kwenye tunda hilo husaidia katika mfumo wa usagaji chakula, kazi inayofanywa katika utumbo mkubwa.
Hata hivyo, tiba katika tunda hupatikana wakati likiwa limeiva na wakati likiwa bichi ambapo ukipata vipande sita vibichi ndani ya wiki moja vinaweza kuondoa mawe kwenye figo na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji.
Kwa wale wanaosumbuliwa na mapigo ya moyo kwenda kwa haraka, Mandai anasema mgonjwa atatakiwa kuchemsha embe bichi likiwa limechanganywa na chumvi, sukari na kisha kunywa ambapo kuanzia hapo ataona mwendo wa mapigo hayo ukianza kubadilika taratibu.
Magome
Magome ya mti huu Mandai anasema kwamba yakichemshwa ni dawa ya homa, ugonjwa ambao unaweza kumsumbua mtu muda mrefu, lakini akipimwa anaambiwa hana malaria japokuwa anaona dalili zote.
Kitaalamu homa huwa haionekani kwenye vipimo na hivyo anachofanyiwa mgonjwa ni kupewa dawa za kutuliza maumivu.
Juisi ya embe
Juisi ya embe inaelezwa kwamba ikichanganywa na maziwa huwa ni kirejesho kizuri cha afya, na hapa Mandai anashauri kwamba ni vyema mnywaji akawa anatumia mara kwa mara.
Hivyo hiyo juisi inaelezwa kwamba ukiwa na tabia ya kuinusa, inasaidia uzuiaji wa utokaji wa damu puani

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!