Friday 4 April 2014

MPINGA ATAKA MADEREVA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mohamed Mpinga.
Madereva  wanaosafirisha abiria jijini Dar es Salaam wametakiwa kufuata sheria za barabarani  ili kupunguza ajali katika maeneo mbali mbali ya Jiji hilo. 
Rai hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini, Mohamed Mpinga, alipokuwa anafungua semina ya mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa Kampuni ya Usafirishaji  Dar es Salaam (Uda) jijini Dar es Salaam.
 


Mpinga alisema asilimia kubwa ya ajali zinazotokea nchini husababishwa na uzembe wa madereva ambao hawataki kufuata sheria ya barabarani. 
Alisema ni lazima madereva wote wajitambue kuwa wao ni watu muhimu katika jamii kwani kazi wanazofanya ni za kuhudumia jamii.
 
Alisifu kazi iliyofanya na Uda ya kuamua kuwaelimisha madereva wa magari yao na kuahidi kuwa Kikosi cha Usalama Barabarani kinachoongozwa na yeye kitahakikisha kinaendelea kutoa elimu hiyo nchi nzima.
 
Mpinga alikishauri Chama cha Wasafirishaji Dar es Salaam (Darcoboa) kuiga mfano wa kuwapa mafunzo madereva wao ili kupunguza ajali na kero kwa abiria ambao wanakutana nazo kutoka kutoka kwa madereva wadaladala.
 
Akitaja baadhi ya sifa zinazomfanya dereva kuwa bora alisema: “Dereva lazima uwe msafi muda wote na utii sheria za barabarani, kuepuka matumizi ya lugha chafu, kutotumia simu, uweza kuona mita 100 mbele na kuonyesha ushirikiano kwa askari wa barabarani.”
 
Aidha, Mpinga alieleza kuwa ana mpango wa kuomba serikali eneo la Morogoro litengwe maalumu kwa ajili ya kufundishia madereva ili kujua sheria zaidi za barabarani.
 
Akimkaribisha Kamanda Mpinga, Mwenyekiti wa makampuni ya Simoni Group Robert Kisena, alisema Uda wamejipanga kuongeza magari zaidi ya 3,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!