Friday 14 March 2014

VIDEO YA OMMY DIMPOZ ILIYOTENGENEZWA HUKO LONDON ILIYOGHARIMU SI CHINI YA DOLA 20,000

Ommy Dimpoz ambae amerudi nchini hivi karibuni kutoka London ambapo alikua ameenda kwa ajili show 2 na kushoot Video chini ya usimamizi wa Gonga Entertainment. Katika Picha Ommy Dimpoz anaonekana ameshikiliwa na Metropolitan Police wa nchini uingereza na hii ni moja kati ya scene ambayo imetumika katika Video ya Nyimbo yake mpya iliyotengenezwa na Director Mr Moe Musa ambaye amefanya kazi nyingi sana na kubwa za wasanii wa Uingereza na Nigeria kama Azonto ya Fuse ODG.


Video hii inatarajiwa kumalizika na kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu ambayo inatarajiwa kuwepo kwenye chanel nyingi na kubwa kutokana na Director na ufanyaji wa Video hii ambapo vifaa vilivyotumika ni modern na vyenye gharama ya juu sana ikiwemo Camera RED pamoja na professional FILM crew waliotumika kushoot video hii.
Video hii imemgharimu OMMY Dimpoz si chini $20,000 za kimarekani ambazo ni kiasi pekee alichomlipa Director huyo na hiyo ukitoa gharama zake nyingine zilizotumika kwenye kusafiri pamoja na kuwepo nchiniUingereza kwa kipindi kizima cha utengenezaji wa video hiyo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!