Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini. Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Wapili Kulia).
Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.
Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.Picha Zote na Saidi Mkabakuli-Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
---
Na Saidi Mkabakuli
Tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji ya uhakika linalowakabili wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mengine inayohudumiwa na mitambo ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini sasa litakuwa historia kufuatia uwekezaji unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukarabati na kupanua mitambo hiyo.
Hayo yalibainika wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa ukarabati na upanuzi wa mitambo hiyo iliyopo mkoa wa Pwani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mhandisi Deusdedit Rwegasira na Mhandisi Emmanuel Makusa ambao ndiyo wasimamizi wa mitambo hiyo, walisema kuwa hali ya ukarabati wa mitambo hiyo inakwenda kwa kasi na inatarajiwa kukamilika kwa wakati, hivyo kutoa ishara njema ya kumaliza tatizo sugu la maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Mhandisi Rwegasira ambaye ni Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu aliambia timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo hadi kukamilika kwake mtambo wake utakuwa na uhakika wa kusafisha na kusambaza takribani lita milioni 100 kwa siku.
Akizungumzia hali ya ukarabati huo, Mhandisi Rwegasira alisema kwamba mpaka sasa Mkandarasi wa mradi huo ameshaanza kazi ya upanuzi wa mitambo hiyo pamoja na kukarabati mitambo ya zamani. Aliongeza kuwa kwa mujibu wa mkataba waliouingia Mkandarasi anawajibika kuongeza mabomba ya usammbazaji kutoka Ruvu Juu hadi Kimara, kuboresha na kuongeza sehemu za kusafishia maji, kukarabati mashine za kuvutia na kusambazia maji.
Aliongeza kuwa Mkandarasi anawajibika kuongeza idadi ya mashine za kuvutia na kusambazia maji ili kufikia lengo hilo kusafisha na kusambaza lita milioni 100 kwa siku.
“Mkandarasi ameshaanza kazi ya kukarabati mitambo yetu ili kutuongezea ufanisi katika kutekeleza uzalishaji wa kutosha wa maji bila kuharibu miundombinu yetu, pia ameanza upanuzi wa mitambo ili kuongeza uzalishaji kama mkataba unavyosema,” alisema Mhandisi Rwegasira.
Kwa upande wake Mhandisi Makusa ambaye ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini alisema kwamba mpaka sasa mradi wa upanuzi na ukarabati wa mitambo yake umefikia aslimia 98 ya malengo iliyoazimiwa.
Mhandisi Makusa alihakikishia timu hiyo ya ukaguzi kuwa kufikia mwezi Juni mwaka huuwa mtambo wake utakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 270 kwa siku ambazo zitasambazwa katika mkoa wa Dar es Salaam na vitongoji vyake kupitia njia ya Ruvu Chini hadi kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Makusa alisema kuwa mradi uliokuwa ukitekelezwa kwenye mtambo wa Ruvu Chini ulijumuisha ujenzi wa jengo la kuhifadhia mashine nne mpya za kusambazia maji, ambapo mpaka sasa mashine mbili zimeshaanza kufanya kazi.
Aliongeza kuwa Mkandarasi aliwajibika kutengeneza jengo jipya la kuchujia maji pamoja na machujio yake manne na kutanua bwawa la kutulizia maji.
“Tunashukuru sana Serikali kwa kusimamia vyema mkandarasi katika kutekeleza kazi hii kwa wakati maana inatupa nguvu ya kuongeza uzalishaji hadi kufikia lita milioni 270 kwa siku,” alisema Mhandisi Makusa.
Ukarabati wa Mtambo wa Ruvu Chini ulifanywa kwa ushirikiano kati wa Kampuni ya Spencon na Ms Degremont.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri anayeshughulikia Huduma za Jamii na Maendeleo ya Idadi ya Watu, alisema kuwa shabaha ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inachagizwa na ari ya Serikali ya Awamu ya nne katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania wanafikiwa na huduma bora na za uhakika ikiwemo huduma ya maji safi na salama.
Aliongeza kuwa kwa kutambua hilo eneo la maji limewekewa mkazo katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.
“Maji ni moja ya eneo la kimkakati katika kipaumbele cha kwanza cha Mpango wetu wa miaka mitano ambapo uwekezaji mkubwa wa miundombinu hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi na maji-taka na umwagiliaji yamewekwa kwa lengo la kumnufaisha kila Mtanzania,” alisema.
Vipaumbele vingine vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/12 – 2015/16 wenye dhana ya kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi Tanzania ni pamona na kilimo, ambapo shabaha imewekwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo ili kuwezesha kujitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje ya nchi; kukuza uzalishaji wa mazao yenye thamani kubwa; kuongeza uzalishaji wa mazao ambayo ni malighafi ya viwandani; kuboresha ufugaji na uvuvi; kukuza kilimo cha misitu; na kuhuisha ubora wa bidhaa zote za kilimo ili kukidhi viwango na mahitaji ya soko.
Pia, maendeleo ya viwanda, hasa vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini: viwanda ambavyo msingi wake ni mazao ya kilimo, mifugo, samaki; na rasilimali misitu; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini; viwanda vikubwa vya mbolea na saruji; kanda maalum za kiuchumi zitakazokuwa na viwanda vya kutengeneza bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na lile la kikanda pamoja na viwanda vya kieletroniki na vile vinavyohusiana na TEHAMA.
Vingine ni pamoja na maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika upatikanaji wa huduma za jamii; na uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.
Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Mpango huu utadumu kwa mwaka 2011/12 - 2015/16 na utakuwa wa kwanza katika mfululizo wa mipango mitatu itakayotekelezwa kwa awamu. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
2011 – 2016 dhana ya kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi Tanzania Vipaumbele hivyo ni: (i) miundombinu hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi na maji-taka na umwagiliaji; (ii) kilimo, kwa shabaha ya kuleta mapinduzi ya kilimo ili kuwezesha kujitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje ya nchi; kukuza uzalishaji wa mazao yenye thamani kubwa; kuongeza uzalishaji wa mazao ambayo ni malighafi ya viwandani; kuboresha ufugaji na uvuvi; kukuza kilimo cha misitu; na kuhuisha ubora wa bidhaa zote za kilimo ili kukidhi viwango na mahitaji ya soko; (iii) maendeleo ya viwanda, hasa vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa nchini:
viwanda ambavyo msingi wake ni mazao ya kilimo, mifugo, samaki; na rasilimali misitu; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini; viwanda vikubwa vya mbolea na saruji; kanda maalum za kiuchumi zitakazokuwa na viwanda vya kutengeneza bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na lile la kikanda pamoja na viwanda vya kieletroniki na vile vinavyohusiana na TEHAMA (iv) maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo maendeleo ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika upatikanaji wa huduma za jamii; na (v) uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.
tangu kufunguliwa kwake tarehe 8 Desemba 1976 mtambo huo uongezaji wa jengo jip “ wakati wa ukaguzi huo mmoja wa katika kutambua changamoto zinazowakabili wakazi wa mkoa huo, Mpango wa Maendeleo uliweka bayana uanzishaji na uendelezaji miradi ya maendeleo ili kutoa huduma za kijamii kwa Watanzania wote
No comments:
Post a Comment