Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kutembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang'ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze
Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kwarihombo,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wapungua mkono wananchi wa Kijiji cha Kwarihombo,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Kijiji hicho,
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea Jogoo kutoka kwa kina Mama wa Kijiji cha Kwamsanja,Kata ya Kibindu
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa Wanachalinze.
No comments:
Post a Comment