Wednesday, 26 March 2014

MAMBO YA SHILOLE HAYO!


“Shilole ni kama anambemenda Nouh lakini ndiyo hivyo, haoni wala hasikii, kila siku wako pamoja kama kumbikumbi,” kilisema chanzo chetu. 
Waandishi wetu waliwafuatilia wawili hao kwa nyakati tofauti na kufanikiwa kuzinasa picha zao walizozipiga katika mikao ya kimahaba.
Baada ya kuzinasa picha hizo, mapaparazi wetu walimtafuta Nouh na kumweka mtu kati kuhusu uhusiano wake na Shilole. 



“Ni kweli ninatoka na Shilole ni mpenzi wangu na sidhani kama nitakuja kuachana naye maana tunapendana sana na nimevutiwa na mavituz yake,” alisema Nouh.
Kuhusu tofauti ya umri wake na ule wa Shilole, Nouh alisema umri huwa haumati katika mapenzi. 

“Mapenzi ni mapenzi na umri utabaki kuwa namba tu, ni vyema mtu ukaongozwa na hisia zako kuliko kuhofia umri wa mtu ndiyo maana miye ninakula vinono,” alisisitiza.
Pia, Nouh alisema hakutarajia kukubaliwa na Shilole baada ya kumtokea walipokutana katika studio moja jijni Dar na sasa wamekolea kwenye penzi motomoto. 

“Nampenda Shishi, nafanya kila njia nimshawishi awe mke wangu wa ndoa,” aliongeza.
Hata hivyo, Shilole alipozungumza na waandishi wetu alipatwa na kigugumizi kukubali uhusiano wake wa kimapenzi na kinda huyo wa Bongo Fleva. 
Shilole alisema Nouh ni rafiki yake kama walivyo marafiki zake wengine.
Waandishi wetu walipomuonesha picha zao walizokuwa wamekaa katika mikao ya kihasarahasara, Shilole aliangua kicheko na kisha akasema: 
 
“Mh! Sina la kuwajibu kama picha zinasema mimi na Nouh ni wapenzi haya.”
Hii siyo mara ya kwanza kwa Shilole kuripotiwa kutoka na Serengeti Boy, siku za nyuma alishawahi kuripotiwa na gazeti dada na hili la Ijumaa Wikienda akisema anapenda kutoka na ‘Serengeti Boys’

PICHA KWA HISANI YA GPL.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!