Maafisa nchini Malaysia wamefichua kwamba wanadhani rubani mwenza katika ndege ya Malaysia iliyotoweka ndiye aliyezungumza maneno ya mwisho kabla ndege hiyo kutoweka.
Maneno hayo bado hayajabainika lakini yanasikika kama -- all right, au goodnight -- ''Kila kitu ki shwari au muwe na usiku mwema'', kabla ya vifaa vinavyowezesha ndege kutambulika katika mtambo wa rader kuzimwa.
Wachunguzi wanaangalia uwezekano kuwa huenda marubani walihusika katika tukio hilo.
Juhudi za kimatifa za kutafuta ndege hiyo pia zinazingatia njia mbili ambazo huenda ndege hiyo ilifuata kwani inaaminika kuwa ilipaa kwa saa kadhaa baada ya mitambo ya mawasiliano kuzimwa
No comments:
Post a Comment