Friday, 21 March 2014

MADAWA TENA! AKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE AKIWA AMEMEZA VIDONGE VYA COCAINE JIJINI DSM



Polisi wamemkamata Abdalah Kaikai (44) aka Mashujaa Udugu Matata, akiwa amemeza vidonge vya cocaine vyenye thamani ya Sh. milioni 75. Kaikai alikamatwa Jumatatu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara tuu baada ya kushuka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.


Mpaka juzi Kaikai alikuwa ameshatoa jumla ya vidonge 82. Kaikai ni mmoja ya wale walioko kwenye list ya polisi ya "most wanted drug traffickers". Kaikai anajulikana zaidi kitaa kwa jina lake maarufu la "Mashujaa Udugu Matata". 

Kamanda wa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya, Godfrey Nzowa, amesema kuwa Mashujaa Udugu Matata alipanda Ethiopian Airlines kutokea Sao Paulo nchini Brazil kuja Tanzania kupitia Addis Ababa. Taarifa za kipolisi zinasema kuwa Mashujaa Udugu Matata ni mkazi wa Buguruni na amekuwa akidai kwa muda mrefu kuwa ni mfanya biashara wa kuuza magari. 

Mwaka 2007, polisi walimkamata Mashujaa Udugu Matata na kuimba mahakama umweke chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa sababu polisi walikuwa na habari kuwa alikuwa anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Wakati huo huyo, wale Watanzania wanne walikamatwa na heroin kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenya Machi 13 wamefikishwa mahakamani ya Kibera jini Nairobi. Awali wamekubali makosa lakini baadae wakayakataa tena makosa (kuepuka kufungwa jela maisha) kwa kigezo kuwa hawakuyaelewa mashtaka yao. 
Mwanasheria John Swaka alidai kuwa watuhumiwa hao walishtakiwa bila kuwepo kwa wanasheria wao kinyume na haki yao ya kuwakilishwa kisheria. Washtakiwa hao ni Bi. Twayba Hashim, Bi. Tina Martin, Bw. Omary Said na Bi. Rehema Ramadhani. Watuhumiwa wote bado wanashikiliwa na polisi hadi Ijumaa ambapo mahakama itasikiliza maombi yao ya bail. 

Habari kwa mujibu wa gazeti la The Citizen

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!