Kwa wale wapitao Mwai Kibaki Road zamani Old Bagamoyo Road watakuwa wanamjua Askari huyu ambaye amekuwa akijituma vilivyo pale darajani Mlalakuwa, Kawe... .. Jamaa alikuwa akimbii mvua, yuko mapema asubuhi, yuko usiku na achoki...labda tu kama ana weakness zake mchana kama vile kwenda kuganga njaa sehemu nyingine kama ilivyo desturi ya askari wengine wa usalama barabarani..
At last, juhudi zimelipa amejishindia Million 2... Naungana na wote alioridhishwa na kazi yake katika kumpongeza...na kumwomba Mkuu angempa hata ka V kamoja zaidi.. ..
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova(watatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage(wapilikushoto)aliyeibu ka kidedea kwenye program ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na kujishindia Sh 2 Milioni. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed maarufu Bonge.
Mfanyakazi wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa tatu kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. 2 milioni kwa askari wa kikosi cha Usalama Barabarani Moses Alphage (wa kwanza kushoto) aliyeibuka kidedea katika program ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini Dar es Salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM. Fedha hizo zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi mbalimbali walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akimkabidhi Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage fedha taslimu Sh. Milioni 2 zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wasikilizaji wa kituo cha Redio Clouds FM kupitia program ya kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalam barabarani jijini dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio.
Askari wa usalama barabarani ,Moses Alphage,akiondoka zake kwa mwendo wa kikakamavu mara baada ya kukabidhiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 2 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova.
No comments:
Post a Comment