SERIKALI ya Burundi imeburuzwa kwenye korti ya Afrika Mashariki (EACJ), kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na utawala wa sheria.
Inadaiwa kumnyang’anya pasi ya kusafiria Rais wa Chama cha Wanasheria Burundi (BBA), Isidore Rufyikiri, baada ya kufanya kikao na waandishi wa habari akizungumzia masuala ya utawala wa sheria, demokrasia na katiba ya nchi hiyo.
Katika shauri hilo lililofunguliwa na Chama cha Wanasheia wa Afrika Mashariki, (EALS), wanamtaka Katibu Mkuu wa EAC kwenda nchini humo kujionea hali halisi ikibidi nchi hiyo isimamishwe uanachama kabisa au kwa muda kutokana na kukiuka vipengele vya mkataba wa jumuiya hiyo
TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment