Wednesday, 12 February 2014

TAARIFA KWA UMMA: MATARAJIO YA KUWA NA VIPINDI VYA MVUA KUBWA, UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA


Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa wametoa taarifa inayoonesha kuwapo kwa mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Unguja, Pemba nk. Utabiri huo ni kuanzia tarehe 11 - 13 Februari. Wanasema uwezekano wa kutokea ni asilimia 60.

Taarifa Na.201402-01
Muda wa Kutolewa: Saa za Afrika MasharikiSaa 11 Jioni
Daraja la Taarifa:Tahadhari
Kuanzia: Tarehe11 Februari, 2014
Mpaka: Tarehe13 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa1. Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24)
2. Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa
pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0
Kiwango cha uhakika:Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa
kuathirika
1. Vipindi vya Mvua Kubwa: Ukanda wa pwani mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya
Unguja na Pemba, Mbeya , Njombe, Ruvuma pamoja na kusini
mwa mkoa wa Morogoro
2. Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa: Pwani ya mikoa ya Tanga,
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba
Maelezo:Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FOBANE” kusini
magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu.
Angalizo:Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya ZiadaMamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo pale itakapobidi

Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!