Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Ripoti ya Kamati ya Mifugo,Utalii, Uwezeshaji na Habari imeitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuipitia upya mikataba ya Ujenzi wa Miundombinu na Uendeshaji wa mitambo ya Digital kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Kampuni ya AGAPE.
Akiwasilisha Muhtasari wa Ripoti ya Kamatihiyo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mlinde Mbarouk Juma amesema kumekuwa na malalamiko mengi na shutuma mbali mbali kutoka kwa makundi tofauti ya jamii kuhusiana na mradi huo hivyo Kamati haikuridhishwa na utendaji wa Kampuni hiyo.
Amesema kuwa Wawekezaji wa AGAPE wameshindwa kufanya kazi na kuitia hasara serikali kwa kutumia wataalamu na rasilimali za serikali na hatimae kushindwa kukidhi mahitaji wa wananchi.
Aidha Kamati imesikitishwa sana na mikataba ya usimamizi na uendeshaji kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na wawekeza wa AGAPE kwamba haufahamiki vizuri katika utendaji wake.
“Kamati imegundua kwamba Shirika la Utangazaji Zanzibar halikushirikishwa kikamilifu katika maamuzi wala mapato yanaypatikana katika mradi huo wa Digital”, alifahamisha Mwenyekiti huyo.
Kamati hiyo pia imesikitishwa na matumizi mabaya ya Jengo la zamani la ZBC ambalo limebadilishwa na kufanywa kuwa nyumba ya starehe kinyume na matumizi yake ambalo hukodishwa na kufanyiwa shughuli mbali mbali za kijamii zikwemo harusi na siku ya kuzaliwa (birth day)na kupoteza haiba yake.
Hata hivyo Kamati hiyo imeshitushwa na taarifa za uvamizi uanoendelea katika shamba la Mifugo Pangeni katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusema kuwa vitendo hivyo vimeshamiri katika maeneo mbali mbali ambavyo huleta hasara kwa serikali.
Akichangia Ripoti ya Kamati hito Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Ali (Jazira) ameomba serikali kuwapatia maposho yao kwa wakati waandishi wa Habari wanaohudhuria katika kikao cha Baraza la Wawakilishi .
Mwakilishi huyo amefahamisha kuwa waandishi wa habari wamekuwa hawapatiwi posho zao kwa wakati kitendo ambacho kinawavuja moyo na kufanya hivyo ni kutowafanyia haki na mshahara wao pia mdogo sana ukilinganisha na kazi wanazozifanya.
No comments:
Post a Comment