Thursday, 20 February 2014

NYUMBA 24 ZACHOMWA MOTO WAKITUHUMIWA KUUA WATU 5


Geita. Zaidi ya nyumba 24 zimevunjwa na kuteketezwa moto Kijiji cha Kilombero, mkoani Geita na wananchi kutokana na mauaji ya Felister Mathias (55), anayedaiwa kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wa ukoo mmoja.
Taarifa zinadai ukoo huo umekuwa tishio kijijini hapo, kwani zaidi ya watu watano wameuawa kwa miezi mitatu kwa kukatwa panga na ukoo huo.
Kutokana na tuhuma hizo, wananchi hao waliingiwa na hasira na kuamua kuchoma nyumba nne za ukoo huo na zingine 20 za wananchi ambao walishindwa kujiunga nao baada ya kupigwa yowe kutokana na kuuawa kwa Mathias.
Akisimlia tukio hilo, mtoto wa marehemu, Christina Charles alisema kabla ya kuuawa kwa mama yake kulikuwa na ugomvi kati yake na mmoja wa wanaukoo hao, ambaye pia ni Katibu wa Sungusungu kwa kile kilichodaiwa ng’ombe wao waliingia kwenye shamba lake. “Kabla mama hajauawa tulikuwa na ugomvi ambao ulitokana na kijana wetu kulisha ng’ombe kwenye shamba la... hali hiyo ilisababisha kuwapo mgogoro ambao tulilipa fidia ya Sh40,000,” alisema Charles.
Charles alisema licha ya kulipa faini, mwanaukoo huyo aliendelea kuwasumbua na kuamua kuhamishia ng’ombe wao eneo la Katoro. Mwenyekiti wa kijiji hicho, Sospeter Bulengeti alikiri ukoo huo ni tishio kwani ni wakorofi na kwamba, ni wahamiaji kutoka Kijiji cha Msalala, Wilaya ya Nyang’hwale.
“Tuliamua kupiga kura zaidi ya watu 300 walishiriki, 20 walipigiwa kura huku ukoo huo ulipata kura nyingi zaidi ya 70,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie alipiga kambi eneo hilo huku akitoa siku 10 wahusika kukamatwa.
Hata hivyo, amri hiyo imesababisha wanaume kukimbia kwa hofu ya kukamatwa kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi. Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ilipokwenda kijijini hapo, ilikuta wanawake wachache na watoto, hali iliyosababisha kushindwa kufanya mkutano wa hadhara.
peke yao ambapo wakati kamati ya ulinzi wilaya inaenda kijijini hapo ilishuhudia kikiwa na wanawake wachache na watoto jambo lililowapa wakati mgumiu wakufanya mkutano wa hadhara na kuamua kuacha.
Pia inaelezwa kwamba tatizo la wananchi kujichukulia sheria mkononi ni uelewa mdogo wa sheria na huku wengine wakidai kuwa jeshi la polis haliwachukulii hatua wanaohusika na uvunjaji wa sheria na pia umbali wa vituo vya polisi jambo linalosababisha kuamua kuwadhibiti waharifu kwa kujichukulia sheria mkononi.

MWANANCHI..

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!