Friday, 21 February 2014

NINI KIFANYIKE KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI? HII NI JANA JIONI AJALI ILIYOPELEKEA WENGI KUJERUHIWA VIBAYA!


WATU wanne wapo katika hali mbaya na wengine saba wamejeruhiwa baada ya lori scania namba T653 BFD  (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda mkuranga.

Kwa mujibu wa shuhuda ya ajali hiyo iliyotokea Mwandege, Dominic Kubhota, ameiambia blogu  ya PAPARAZIHURU  usiku huu kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ovateki isiyotumia akili ya lori hilo .

Majeruhi hao wamefikishwa katika hospitali ya Mkuranga, lakini muda mfupi baadaye walianza kukimbizwa kuleta dare s salaam kw amatibabu zaidi.
Abiria wawili waliokuwa mbele  ya daladala walikatika miguu.
 
Majeruhi wengine walioweza kuzungumza ni:
Mustafa mfungapoa wa mkuranga
Abdul Ally wa mwandege
Ramadhani rajab
Theofrida Mwinuka ( alikuwa mbele amevunjika miguu)
Jamal  mbaraka ( aliyekwanguka ngozi ya kichwa)
Abraham Mohamed

Swalehe salum

HABARI NA PICHA KWA HISANI YA PAPARAZ BLOG.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!