Serikali imetangaza rasmi kutupilia mbali mikakati ya wajumbe wa Bunge la Katiba ya kujiongezea posho kutoka Sh300,000 mpaka Sh500,000 kwa siku.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba amesema serikali haina fedha za nyongeza za posho kama wajumbe wa bunge hilo wanavyotaka.
Nchemba amesema kama kuna wajumbe ambao wanataka kuongezewa posho na wanafikiri posho wanapewa sasa, haiwatoshi ni bora waache shughuli hiyo na kwenda kufanya kazi nyingine.
“ Kama kuna wajumbe wanafikiri kwamba Sh300,000 haziwatoshi ni bora wafungashe virago,” amesema.













No comments:
Post a Comment