Friday 7 February 2014

MTANZANIA ALIYETISHIA KUVUJISHA SIRI ZA MKE WA ZUMA KURUDISHWA NCHINI



Mkuu wa Tawi la Uchunguzi wa Kesi, katika Jimbo la Kwa Zulu-Natal, Brigedia Clifford Marion, alisema Stephen Ongolo ambaye ni raia wa Tanzania anayekabiliwa na madai ya kutishia kutoa siri za mke wa Rais Jacob Zuma, Nompumelelo Ntuli (MaNtuli), huenda akarudishwa nchini na kuzuiwa kuitembelea Afrika Kusini milele.

Akiongea wakati wa kusikilizwa kesi hiyo katika Mahakama ya Camperdown, jijini Durban, Brigedia Marion alisema “Ongolo si raia wa Afrika Kusini na Viza yake inamalizika Februari 18 mwaka huu na atarudishwa nchini mwake Tanzania na hatarudi tena Afrika Kusini,” alisema Marion.


Kuhusiana na tuhuma dhidi ya Stephen Ongolo, Brigedia Marion alitoa ushahidi kuwa Ongolo amekuwa akituma ujumbe mfupi kwenye simu ya MaNtuli, akimtishia kuwa atatoa siri kuhusu uhalali wa mtoto wake (MaNtuli).

Inadaiwa kuwa Ongolo katika ujumbe wake alidai kuwa mtoto mmoja wa MaNtuli si wa Rais Zuma.

Kabla ya kukamatwa, Ongolo alikwenda katika vyombo vya habari kadhaa vya nchini humo na kudai kuwa, anafahamu siri nzito kati ya MaNtuli na Phinda Thomo, aliyekuwa mlinzi wa MaNtuli.

Thomo, alikutwa amejiua mwaka 2009 bafuni kwake, lakini Ongolo anadai kuwa Thomo hakuuawa na badala yake, kifo chake kilipangwa kutokana na uhusiano wa siri kati yake na MaNtuli.

CREDIT..DAR 24

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!