Saturday, 1 February 2014

KAMATI YA MAADILI YA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) YAIADHIBU TIMES FM BAADA YA MTANGAZAJI MAARUFU DIDA KUGEUZA KIPINDI CHAKE CHA TAARABU KUWA KIPINDI CHA UGONVI BINAFSI



KAMATI ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), imesema mtangazaji Hadija Shaibu maarufu Dida wa Radio Times FM ya Dar es Salaam, alitumia chombo hicho vibaya kumshambulia binafsi msanii wa muziki wa taarab, Karya Temba katika kipindi cha cha ‘Mitikisiko ya Pwani.’
Aidha, Kamati imesema Dida aligeuza kipindi anachorusha redioni hapo kuwa cha ugomvi binafsi kati yake na mlalamikaji ambaye ni Karya na kwamba alichochea wasikilizaji kutuma meseji za kejeli kwa mlalamikaji jambo ambalo sio lengo la usajili wa kituo hicho.
Vile vile Kamati hiyo imesema redio hiyo ilikiuka maadili ya utangazaji kwa kurusha kipindi kinachoshutumu watu kwa kutumia kabila lao na kilikuwa na maudhui ya udhalilishaji wa kijinsia, kinyume cha maadili na kanuni bora za uanahabari.


Maelezo hayo yalitolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakati akifafanua juu ya malalamiko ya msanii huyo akidai kipindi hicho kilimdhalilisha na kumharibia sifa kama mwanamuziki.
Jaji Mihayo alisema baada ya kamati kusikiliza pande hizo mbili, inaagiza redio hiyo kumwomba radhi mlalamikaji kupitia kipindi hicho katika vipindi vitatu mfululizo kuanzia Februari 5 na maudhui ya radhi hiyo yataridhiwa na MCT.
Alisema kituo hicho, pia kimlipe mlalamikaji Sh 500,000 kama gharama za kutayarisha malalamiko na kimuandikie barua ya kumwomba radhi ndani ya wiki moja kuanzia jana na nakala kutumwa MCT.
Katika shauri hilo namba 28, 2013, Temba analalamika kushambuliwa, kukashifiwa na hata kubaguliwa na mtangazaji huyo katika kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani anachokirusha redioni hapo

HABARI LEO.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!