Friday, 14 February 2014

DIWANI WA KATA YA MBWENI BONIFACE MNYACHIBE(CCM)AFARIKI DUNIA



Marehemu Boniface Mnyachibwe Enzi za Uhai wake
TANZIA

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inapenda kutangaza kifo cha Diwani
wa kata ya Mbweni Mh. Boniface Mnyachibwe kilichotokea leo ghafla saa
tatu asubuhi.
Tunatoa pole kwa familia yake, wakazi wa Mbweni, Wananchi wa Kinondoni pamoja na Chama chake cha CCM.
Mchango wake mkubwa ktk kuboresha maisha ya wakazi wa Mbweni na
Kinondoni kwa kujituma na uadilifu kamwe hautasahaulika. Aidha, kifo
chake cha ghafla leo wakati jana tulikuwa naye mpaka saa moja na nusu
jioni kwenye vikao vya bajeti ni uthibitisho wa uzalendo wake na mapenzi
yake kwa anaowawakilisha na Kinondoni kwa ujumla.
Dua zetu na sala zetu ziende kwa familia yake na wote aliokuwa anawawakilisha.
Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi.Imetolewa na Manispaa Ya Kinondoni

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!