Monday, 3 February 2014

ALIYEKUWA KIGOGO WA BOT ATUPIWA VYOMBO VYAKE NJE, ANGALIA HAPA

Picha na silivan Kiwale 

Mkurugenzi wa zamani wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
 Elisa Issangya, akiwa ameduwaa baada ya vyombo vyake kutolewa
 nje ya nyumba na Kampuni ya Udalali ya Mwafrika. 
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa zamani wa Fedha wa Benki
 Kuu Tanzania (BoT), Elisa Issangya amejikuta akitupiwa vyombo
 vyake nje na Kampuni ya Udalali ya Mwafrika kwa kile kilichoelezwa
 kutakiwa kuondoka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.

Nyumba hiyo iliyoko Mtaa wa Ruhinde Block 2 Plot 294 eneo
 la Ada Estate wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, inaelezwa
 kuwa inamilikiwa na BoT.
Akizungumza nyumbani kwake baada ya kutupiwa nje vifaa vyake
 Issangya alisema: “Nimeshtukizwa na maofisa wa Kampuni ya Udalali 
ya Mwafrika kuingia ndani kwangu na kuniomba nishirikiane nao kutoa 
vitu vyangu nje.

“Maofisa hao wa Kampuni ya Mwafrika walifika nyumbani kwangu 
asubuhi na kunionyesha barua kutoka BoT ya kunitaka kuvitoa vyombo 
vyangu nje, sikukubaliana nao, nikaamua kwenda polisi kutoa
 taarifa,” alisema.
Alisema wakiwa polisi na ofisa mmoja wa kampuni hiyo aliyemtaja
 kwa jina moja la Gama ambaye alikuwa akimweleza kuwa
 watamuelewesha
 suala hilo baada ya kuondoa vyombo hivyo , lakini waliporejea nyumbani
 kwake, walikuta vyombo vyote vimetupwa nje.
Issangya alisema kitendo cha kutupiwa vifaa nje ni udhalilishaji kwani 
walitakiwa kwenda nyumbani kwake wakiwa na barua ya mahakama
 ya kuwaruhusu kufanya hivyo.
“Nimeshangaa hatua hiyo wakati mpaka sasa kesi yangu ya kudai
 haki zangu ipo mahakamani, wangesubiri mpaka hukumu ikitolewa
 ndipo waje na uamuzi huu,” alilalamika Issangya aliyeteuliwa kushika
 nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha wa BoT mwaka 2000 kabla
 ya kusimamishwa 2008.
Alipoulzwa sababu za kufanya hivyo wakati suala la mlalamikaji bado
 liko katika vyombo vya sheria na uamuzi wa shauri haujafikiwa
 Ofisa wa Kampuni hiyo ya Udalali, Joseph Gama alisema kuwa 
wanatekeleza maagizo ya tajiri wao na si vinginevyo.
“Sisi tunafanya kazi kwa amri ya tajiri wetu, hatuwezi kufanya mambo
 kinyume na maelekezo, tumeelekezwa na huu ni utekelezaji wake,” alisema

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!