Thursday, 30 January 2014

YAYA TOURE, D`BANJI WAUNGANA NA KIKWETE KWENYE KILIMO


KAMPENI inayohamasisha vita dhidi ya umaskini kwa kutumia kilimo iliyoasisiwa na Rais Jakaya Kikwete na Shirika la One la Marekani, imeungwa mkono na msanii D'Banj wa Nigeria pamoja na mchezaji wa Manchester City, Yaya Toure.
Hiyo ni baada ya D’Banj kushirikiana na washirika wa Kilimo wa Afrika katika uzinduzi wa kampeni ya 'Shiriki Kilimo' (Do Agric) kwenye kongamano la Umoja wa Afrika.



Kampeni hiyo inalenga kuwasaidia watu zaidi ya milioni 85 barani Afrika kutoka katika lindi la umasikini kupitia uwekezaji maalumu katika kilimo na sera za kilimo za Maputo zilizoboreshwa.
D'Banj alikuwa mmoja wa waliozungumza Addis Ababa jana wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo yenye lengo la kuwahamasisha viongozi wa kisiasa kutumia sera nzuri zitakazonyanyua uzalishaji, kuongeza kipato na kuondoa mamilioni ya Waafrika kutoka katika umasikini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, D’Banj alisema kuwa anatambua kuwa zipo fursa nyingi katika kilimo na ambazo hazijafanyiwa kazi ipasavyo. Alisema fursa hizo zikitumiwa vema zinaweza kutengeneza ajira kwa mamilioni ya Waafrika waliopo na wasiopo mashambani.
"Nataka Waafrika kufahamu kilimo ni msingi mzuri wa uchumi ambacho kinatakiwa kutiliwa mkazo na kuleta mabadiliko katika uchumi wa wananchi na nchi na pia tukitilia mkazo tunaweza kuilisha dunia nzima kwa ujumla sisi kama Waafrika," alisema D'Banj.
Kwa upande wake mchezaji wa timu ya Manchester City, Toure alisema wakati viongozi wengine wa Kiafrika wakitoa kauli zenye nia njema, kwa sasa ni nchi 8 tu zililizotimiza ahadi zake za kuwekeza 10% ya bajeti za nchi katika kilimo.
"Kwa hiyo ni muhimu kufanya zaidi na kwenda mbele zaidi. Kilimo sio muhimu pekee, pia ni lazima. Kilimo kinalipa," alisemaToure.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na asasi mbalimbali za kiraia zikiwemo Pan African Farmers Association (PAFO), Action Aid International , Acord International, Oxfam na Alliance for Green Revolution In Africa (AGRA) mbali na asasi hizo mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure pia ametia saini kuunga mkono uhamasishaji huo

HABARI LEO

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!