Wednesday, 1 January 2014

WATU WA 3 WAMEKUFA NA WENGINE KUJERUHIWA MAPANGA KATIKA MKESHA WA MWAKA 2014


Juma fungo mkazi wa kiwalani Relini jijini Dar es sal;aam ambaye alipigwa mapanga katika paji la uso na kundi la watu waliokuwa wanasherekea mwaka mpya , inasemekana watu hao walimpora vitu kadhaa ikiwa ni pamoja na simu  pesa na kitambulisho cha kazi.


Watu wa 3 wamekufa  papo hapo kwa kupigwa risasi na wengine kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga  katika mkesha wa  mwaka mpya  2014.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la Pugu  Kigogofreshi barabara ya chanika usiku wa kuamkia  mwaka mpya  ambapo watu hao  wa 3 walipigwa  risasi na kundi la watu waliokuwa katika sherehe za mwaka mpya, kundi la watu hao linalosadikiwa kuwa ni la vibaka ,  walitanda barabarani na kuzuia  magari kupita.
 kwa mujibu ya askari polisi waliokuwa katika doria  miili ya watu 3 ilipelekwa katika hospitali ya Amana  pamoja na majeruhi kadhaa waliojeruhiwa kwa risasi.

 Mwandishi wa habari hizi akiwa katika hospitali ya Amana ambaye pia  kijana wake  aliejeruhiwa kwa panga usoni katika sakata hilo.

Katika eneo la kiwalani kulikuwa na matukio ya kupora  simu fedha na kupigana mapanga kwa kila mtu aliekutwa nje ya nyumba yake  na pia kwenye nyumba za starehe.
Inasemekana kundi hilo kubwa la vibaka  lililotokea sehemu ya vituka.
  


Vurugu hizo ziliendelea mpaka eneo la kiwalani relini nyumba zilzopo katika maeneo hayo  zilivamiwa na kundi hilo la watu wakitumia silaha za mawe ,mapanga ,fimbo na pia uporaji wa simu na pesa ulitawala,  kundi hilo pia lilivamia maeneo ya mpakani bar,yombo matangini pia walipiga watu kwa mapanga  eneo la ccm kata ya kiwalani.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia vijana 2 walioletwa na askari katiaka hospitali ya amana kufuatia vurugu zilizokuwa zikiendelea wakati wa sherehe za mwaka mpya,  mmoja ya majeruhi hao  akiwa na risasi mguuni .
  

Picha na blog ya mzuka wa fungo




No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!